Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 3 3
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kiinjili inaanza na dhana kwamba kanuni ya wokovu daima ni “kwa neema kwa njia ya imani.” Hakikisha kwamba kila mwanafunzi anaelewa ukweli huu wa msingi.
8 Ukurasa 50 Kipengele namba I-D-2
Ufafanuzi kuhusu Ibada
9 Ukurasa 51 Kipengele Kipengele namba II
Maneno makuu ya kibiblia, saha la Kiebrania na proskyneo la Kiyunani, yanasisitiza tendo la kusujudu. ~ E. F. Harrison, “Worship.” Evangelical Dictionary of Theology . uk. 1192. Ibada ni kumwitikia Mungu kwa kutambua kikamilifu nafasi yake kama Anayestahili kabisa ibada, utii, utumishi, shukrani, na sifa. Zab. 95:6 – Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba (rej., Law. 26:1; Kum. 26:10; Zab. 138:2; Mt. 4:9-10). Neno la msingi wa ibada: tunamwabudu Aliyefunuliwa kwetu. Kama si kusikia Neno la Mungu tusingeweza kumwabudu kwa sababu tusingemjua. Anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa. Tunaweza kumwitikia kwa sababu tu amejifunua. Yn. 1:18 – Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua Msingi wa kiagano wa ibada: tunaabudu kwa njia ya Kristo Yesu (Waebrania). Ibada ya Kikristo ni tofauti kwa kuwa ina msingi katika Kristo. Pazia limepasuliwa. Tuna njia ya moja kwa moja kwa Baba kupitia Kristo Yesu. Tukimtukuza Mungu Baba kupitia yeye. (Ebr. 10:20 BHN – Yeye ametufungulia njia mpya, njia ya uhai, kupitia lile pazia, yaani mwili wake mwenyewe…) Msingi wa kijumuiya wa ibada: ukuhani mtakatifu (ibada daima ni ya ushirika kwanza, ndiposa inakuwa ya mtu binafsi). Ebr. 10:25 – Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. Baadhi ya Mawazo Muhimu
Made with FlippingBook - Share PDF online