Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 3 7
THEOLOJIA YA KANISA
yaliyoulizwa na wanafunzi wako, na uangalie mambo yoyote ambayo yanaweza kukutoa kutoka kwenye msisitizo wa kweli muhimu na mambo makuu ya somo.
Ibada kwa Mungu ni dhana kuu, na ili kuielewa vya kutosha dhana ya Kanisa katika ibada, unaweza kuwaelekeza wanafunzi kwenye dhana za jumla zinazohusiana na neno hilo. Neno letu “kuabudu au ibada” limechukuliwa kutoka kwa neno la zamani la Kiingereza, “ worthship ” (kustahili) ambalo lilirejelea kustahili kwa mtu kupewa heshima au kutambuliwa kulingana na thamani ya hadhi au nafasi yake. Kuna maneno kadhaa yanayotumiwa katika Maandiko yanayohusiana na wazo la ibada, na labda maneno muhimu zaidi ni neno la Kiebrania saha na la Kiyunani proskyneo . Dhana hizi zinahusianishwa kwa ukaribu na vitendo vya kimwili vya kuinama, kusujudu mbele ya mtu mwingine, kitendo cha kutoa heshima kubwa au kumsujudia mtu mwingine au kitu fulani kutokana na hisia ya heshima kubwa, kicho, na hali ya kutambua. Uelewa huu wa ibada unaohusishwa na kusujudu, wa kumsujudia mwingine unaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na maadili au mazoea ya kijamii yaliyofanyika kwa lengo la kutoa heshima ifaayo kwa mtu anayetambulika na kukubaliwa kuwa anastahili (Mwa. 18:2), cheo kilichotukuka ambacho mtu angeweza kuwa nacho katika nafasi yake ya maisha (1 Fal. 1:31), au cheo na/au nafasi ambayo mtu binafsi alikuwa nayo katika muktadha wa jumla wa familia (Mwa. 49:8). Tendo hili la kusujudu, liwe ni tendo la kimwili tu au utii na ukiri kwa ndani, linaweza pia kutumika kwa viumbe vinavyopewa heshima kama miungu, iwe sanamu za watu au taifa (k.m., Kut. 20:5) au kwa Yahweh Mungu (Zab. 2; Kut. 24:1). Mungu wa Biblia ameweka wazi kwamba hatashiriki utukufu na heshima anayostahili na miungu mingine yoyote, ambao kwa kweli hawakuwa miungu hata kidogo isipokuwa walikuwa ama kazi za akili na mikono ya waabuduo au mashetani wanaotafuta kuiba utukufu ulio wa Mungu peke yake (Kut. 20:1-3; Isa. 14; Kum. 8:429; Isa. 42:8). Kuitolea miungu ya uongo utukufu, heshima, na utii ambao ni Mungu pekee ndiye anayestahili ni kilele cha kiburi na dhambi; Mungu, kwa sababu ya thamani yake isiyo na kikomo na heshima yake isiyo na kifani, hatavumilia tendo la aina hii, haijalishi kwamba linafayika kwa hiari, pasipo hiari au kwa kulazimishwa. Zaidi ya yote, utukufu wa Mungu usio na kikomo unamaanisha pia kwamba Yeye ni Mungu mwenye wivu (Kut. 20:5), si kwa maana ya kwamba Mungu ana choyo na ubinafsi wa kutaka kutambuliwa peke yake.
20 Ukurasa 63 Kipengele namba I
Made with FlippingBook - Share PDF online