Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 3 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
Kinyume chake, Mungu ana wivu kwa maana ya kwamba hakuna mtu ambaye anatakiwa kujipa utukufu mwenyewe na hakuna kitu ambacho kinapaswa kujipa utukufu chenyewe; Uzuri wa Mungu na ukuu wake hauna kifani, na kumruhusu mtu yeyote kumnyang’anya heshima yake itakuwa aina mbaya zaidi ya dhambi na makosa. Kati ya matendo yote yaliyopotoka zaidi ya kumnyang’anya Mungu haki yake halali ya kupata utukufu wote, jaribio kichaa la Ibilisi linaonekana kuwa baya zaidi (Isa. 14:12-20). Maandiko yanarekodi jaribio lake lisilo na maana la kupokea sifa na utukufu kutoka kwa Kristo, ambao ni Mungu peke yake anayestahili (Mt. 4:9), na katika nyakati hizi za mwisho, wawakilishi wake watatafuta sifa ile ile ya kipumbavu (rej. 2 Thes. 2 na Ufu. 13:4). Kwa sababu Mungu ana utukufu usio na kikomo, ibada yake (yaani, kustahili kwake) haiwezi kuwekewa mipaka kwa maana tu ya kile kinachotendeka ndani ya hekalu, au kwa tafsiri ya kile ambacho Kanisa linafanya pale linapompa Mungu heshima kupitia sifa na shukrani zake. Si tu kwamba tunaweza kujumuisha matendo yote ya watakatifu na malaika katika kukiri utukufu wa Mungu katika ibada (rej. Zab. 150; 138:2; 1 Sam. 1:3), bali pia kazi zote mbinguni na duniani, kutia ndani mbingu zote, sayari zote, aina zote za uhai na viumbe, kimsingi kila kilichoumbwa kinampa Mungu utukufu na ibada kinapotimiza kusudi la kuumbwa kwacho. (Zab. 135:6 na Ufu. 4:11). Kama utakavyoona katika somo hili, Mungu aliifanya ibada yake kuwa tajiri zaidi na kujidhihirisha zaidi kupitia umwilisho wa utukufu wake mwenyewe katika nafsi ya Yesu Kristo (Yoh. 9:38; 20:28; Ebr. 1:6; Ufu. 5:6-14). Mungu wetu, ambaye haelezeki katika uzuri na ukuu wake, anastahili kusifiwa ndani ya Mwanaye na kupitia Mwanaye, ambaye anapaswa kuabudiwa pamoja na Baba kama Mwokozi na Bwana wetu (Yoh. 5:22-23). Linaweza kuwa jambo lenye manufaa kusisitiza hapa kwamba Kanisa la kwanza, kizazi cha jumuiya ya kwanza ya Wakristo huko Yerusalemu, lilitegemea sana mizizi na mwelekeo wake wa Kiyahudi katika nyanja zote za ibada, hasa kwa maana ya kwamba Kanisa lilitumia Agano la Kale kama Neno lake lenye mamlaka. Ushirika huu wa awali ulilenga kukiri kwamba Yesu wa Nazareti ndiye Masihi aliyeahidiwa na kwamba wokovu wa Mungu na utawala wake umekuja kupitia maisha ya mtu huyo
21 Ukurasa 66 Kipengele namba II
Made with FlippingBook - Share PDF online