Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 3 9

THEOLOJIA YA KANISA

Yesu Kristo na kupitia kifo na ufufuo wake. (Imani hiii juu ya Yesu, zaidi ya yote, pengine ndiyo iliyowatofautisha na wenzao wa ibada ya Kiyahudi). Kwa hiyo, ibada ya Kanisa la kwanza ilijikita katika maudhui tofauti (Yesu kama Masihi na Mwokozi), lakini inafanana sana na mwelekeo wa Kiyahudi, japo ilijumuisha nyongeza muhimu na kuu ya Ekaristi (yaani, Meza ya Bwana) katikati yake, (Mdo. 2:42, 46) pamoja na sala zinazotolewa kwa Mungu katika jina la Bwana Yesu (Mdo. 4:24-30). Ingawa tunaona ushahidi wa kukusanyika kwao kuomba, kuwa na ushirika, na kusikia Neno la Mungu likihubiriwa na kufundishwa (k.m., Mdo. 2:46; 5:42), jumuiya ya kwanza ilibadilisha siku yake ya huduma kutoka Sabato hadi Jumapili, siku ya kwanza ya juma, tangu Bwana Yesu alipofufuliwa siku ya kwanza ya juma. Ingawa wasomi hawakubaliani kuhusu asili ya mfumo wa ibada ya Kanisa la mitume la kizazi cha kwanza, kuna makubaliano kwamba muundo huo ulikuwa rahisi na wa dhati katika kumcha Mungu. Ushahidi wa Agano Jipya na maandishi yasiyo ya kikanoni unaonyesha kwamba ingawa ibada haikuwa na utaratibu wa kimfumo au mwelekeo unaofanana, kiini na kitovu cha huduma za Kikristo kilikuwa ni adhimisho la Meza ya Bwana katika Siku ya Bwana. Kitabu The Didache (Mafundisho ya Mitume 12, takriban miaka ya 95-150), chanzo cha thamani na cha mapema kabisa chenye ushahidi kuhusu imani ya Kikristo na utendaji wa Kanisa la kwanza, kinatupatia simulizi tele za jinsi Wakristo wa kwanza walivyoadhimisha Ekaristi, kikieleza kwa kina sala walizotumia, maelekezo ya kiliturujia ambayo yalihitaji kufuatwa, pamoja na namna za sala zinazopaswa kusali. Walitoa muda kwa ajili ya maombi ya wazi katika nyakati fulani za ibada (liturujia). Kabla ya mwamini yeyote kusherehekea Meza ya Bwana, kuungama dhambi kulihitajika kwa wote waliotaka kushiriki katika sherehe yao (Didache 14:1). Uyahudi wa ibada ya Kanisa la kwanza ulikuwa dhahiri kabisa, na kwa sababu hiyo, halikuwa jambo geni kusikia na kushuhudia miongozo na mielekeo ya sifa na ibada ya Kiyahudi katikati ya makusanyiko ya kwanza ya Kikristo. linaweza kuwa jambo la kuvutia kwako na wanafunzi kujua kidogo kuhusu mwanzo wa dhana ya liturgia, utaratibu maalum na ratiba ya muundo wa ibada inayotumiwa katika makanisa mengi leo duniani kote. Mmoja wa mababa wa mapema wa Kanisa, Justin Martyr, anabainisha katika kitabu chake cha First Apology ambacho aliandika karibu katikati ya karne ya pili, maelezo ya wazi ya

 22 Ukurasa 68 Kipengele namba II-B

Made with FlippingBook - Share PDF online