Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 4 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
ibada ya Kikristo, pamoja na Meza ya Bwana (au ekaristi, “shukrani”), ambayo pia inarejelewa katika The Didache (14:1). Justin anaelezea huduma ya ibada ya Kikristo katika karne ya pili kama usomaji wa “kumbukumbu za mitume” (yaani, Injili), pamoja na Manabii (vitabu vya Agano la Kale) vilisomwa kwa sauti “kwa kadri muda ulivyoruhusu” ( First Apology , 67). Maelezo ya Justin yanaonyesha kwamba makanisa yalikumbatia utaratibu mahususi wa ibada zao kutokana na mapokeo yao ya pamoja, ingawa ulikuwa utaratibu rahisi sana. Kutokana na ushahidi tunaona pia kwamba waamini waliobatizwa walikusanyika na kusherehekea Meza ya Bwana, iliyohusisha mlo kamili ambao watu wote walishiriki, lakini mlo huo ulitenganishwa na sherehe ya Meza ya Bwana mapema sana katika historia ya Kanisa (Klementi wa Aleksandria, Paedagogos 2:1; Stromata 3:2; Tertullian, Apology 39); Mlo huu unaohusishwa na Meza ya Bwana ulikuja kuitwa “karamu ya agape,” yaani, karamu ya upendo, lakini kulingana na kumbukumbu zetu, karamu hii ilikufa kufikia karne ya nne kwa sababu ya matatizo makubwa ya tabia yaliyohusishwa nayo (Augustine, Barua kwa Aurelium 22:4). Wakiwa wameathiriwa sana na maadhimisho ya sherehe za Kiyahudi mwaka mzima, Wakristo walitokeza mapema wazo la “mwaka wa Kanisa,” unaofanana na mwaka wa Kiyahudi. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa wazo la kisasa la “mwaka wa kiliturujia,” ambayo ilikuwa juhudi ya Kikristo ya mapema ya kutenga mwaka kupitia kusimuliwa tena na tena kwa hadithi ya Kikristo kupitia mfululizo unaoendelea wa matukio matakatifu na sherehe. Ni jambo linalokubaliwa ulimwenguni kote kwamba uteuzi halisi na ujumuishaji wa sherehe na sikukuu fulani ulifanyika hatua kwa hatua kwa muda fulani. Kwa mfano, sherehe za Krismasi na Epifania, ingawa ni sehemu kuu ya hadithi ya Kikristo, zilikuja kuongezwa kwenye kalenda ya kiliturujia mnamo karne ya nne, na kalenda ya sasa iliendelea kuongezewa matukio na maboresho hadi kukamilika kwake mwishoni mwa karne ya sita. Msisitizo huu wa liturujia unapaswa kuonekana kama matokeo ya Ukristo kutegemea mizizi na mwelekeo wa Kiyahudi, ambao umetumika kama msingi na chanzo cha liturujia ya kisasa.
Katika kushughulika na dhana za kipindi hiki cha majadiliano, ni muhimu kwamba ufanye tofauti fulani kwa wanafunzi ambazo tunatumai zitawawezesha kukumbuka mambo muhimu na ya msingi yanayohusiana na mada ya Kanisa katika ibada . Kazia kwa wanafunzi kwamba ingawa Biblia inarejelea kanuni na mielekeo fulani
23 Ukurasa 70 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Share PDF online