Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 1
THEOLOJIA YA KANISA
inayohusiana na kumwabudu Mungu, hakuna kanuni, vielelezo vilivyowekwa, au ratiba za desturi zilizoamriwa zinazohusiana na ibada. Pamoja na ukweli kwamba Meza ya Bwana na ubatizo vinahusianishwa na ibada ya Kanisa, tangu mwanzo kabisa wa ibada ya Kanisa, halikutumia wala kutafuta mfumo fulani mahususi na wa lazima kwa ajili ya makusanyiko yote ya ibada. Ingawa kutoka katika Agano Jipya na maandishi ya kihistoria yasiyo ya kikanoni tunaweza kugundua mapokeo ya uhakika yanayojitokeza katika makanisa ya mitume ambayo yalizaa kalenda ya kiliturujia ya leo, hapakuwa na wakati ambapo kila sehemu ya ibada iliamuliwa na kupangwa kabla. Katika mjadala wako, hakikisha kwamba unaangazia msisitizo huu kuhusu ibada ya Kanisa ambao unaonyesha uwepo wa ibada zilizojumuisha uaminifu wa dhati na wa kina kwa mapokeo ya mitume, wakati huo huo, zikiruhusu mtazamo mpya wa uhuru na kutofuata mpangilio fulani maalum. Hili ni muhimu kwa ajili ya uelewa wa yote ambayo Biblia inaeleza kuhusu Kanisa katika ibada. Hakikisha kwamba unatofautisha kati ya mwitikio wa Kanisa katika ibada yake kwa Mungu (ibada kulingana na matokeo yake) na uzuri wa Bwana, tabia yake na kazi yake katika Yesu Kristo (ibada kulingana na sababu yake). Kwa bahati mbaya, baadhi ya mijadala ya ibada imejikita zaidi kwenye namna tunavyoabudu badala ya sababu zinazotufanya tuabudu . Ingawa yote mawili ni muhimu katika kuelewa wito wa Kanisa kama ukuhani wa kiibada wa waamini, ni muhimu kwamba lengo libaki kwa Mungu ambaye tunamwabudu, na sababu ya wazi kwa nini sisi ni jumuiya ya kiibada. Ni pale tu dhana hizi zinaporejelewa na kuwekwa wazi ndipo tunaweza kufikiria kiusahihi njia tunazopaswa kumkaribia Mungu. Sababu ya ibada lazima itangulie dhana ya “ nini” na “ namna gani” ya kuabudu. Kauli hii haipaswi kueleweka kama rufaa ya kudharau umuhimu wa majadiliano juu ya mwitikio wa wanadamu kwa Mungu. Hata hivyo, ni kusisitiza kwamba umuhimu wa ibada unatokana na kuelewa kwamba Mungu anastahili kusujudiwa na kupewa utii wetu. Majadiliano ya ibada yanapaswa kuanza na kumalizika katika msingi wa Mungu na sio msingi wa wanadamu.
24 Ukurasa 71 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Ingawa kuna matokeo mengi binafsi kwa fundisho hili la ibada, itakuwa muhimu kwako kama mkufunzi kuwasaidia wanafunzi kutunza asili ya ushirika katika maswali na masuala yote. Tabia ya kugeuza mjadala kuhusu Kanisa katika Ibada kuwa “mimi katika ibada” imeenea sana, na uwezo wako, katika mapitio na
25 Ukurasa 73 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - Share PDF online