Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 5
THEOLOJIA YA KANISA
Kanisa kama Shahidi
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu kwenye Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 3, Kanisa kama Shahidi . Lengo la jumla la somo hili la moduli hii ya Theolojia ya Kanisa ni kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa nyanja mbalimbali za Kanisa katika ushuhuda wake kwa habari ya Kristo na Ufalme wake. Tunaanza somo hili kwa kuzingatia baadhi ya vipengele muhimu zaidi vya fundisho la uchaguzi jinsi linavyomhusu Yesu Kristo kama Mtumishi Mteule wa Mungu. Katika Yesu Kristo, Mungu amejichagulia Mwokozi na Bwana ambaye kupitia kwake alijidhihirisha kwa ulimwengu, na kukomboa watu kwa ajili yake mwenyewe. Wenye haki huchaguliwa kwa sababu ya muungano wao na Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, kwa imani. Pia tutazingatia hasa jinsi uchaguzi wa Mungu unavyohusiana watu wake wateule Israeli na pia Kanisa. Kwa kutumia uteuzi wa Mungu kwa Israeli na Kanisa kama msingi wa dhana hii, basi tutaangazia kwa ufupi uhusiano wa uchaguzi wa Mungu wa waamini binafsi “katika Kristo,” yaani, kuhusiana na Kristo wanaposhikamana naye kwa imani. Sehemu ya pili ya somo hili inaangazia Agizo Kuu, agizo ambalo Yesu ametoa kwa Kanisa la zama hizi kushuhudia habari zake na ahadi ya ufalme kupitia imani katika damu yake iliyomwagika. Katika sehemu hiyo tutaona jinsi Agizo Kuu linavyotoa muhtasari wa jumla wa ushuhuda wa Kanisa wenye sehemu tatu, ambao unalituma ulimwenguni kufanya wanafunzi. Tutazingatia jinsi Kanisa linavyotimiza agizo la Kristo kwa kutii wito wa Yesu wa kuwahubiria Injili waliopotea, kwa kuwabatiza waamini wapya katika Kristo (kuwajumuisha kama washirika katika Kanisa), na kwa kuwafundisha waongofu wa kweli kutii yote ambayo Kristo amewaamuru. Kanisa limeitwa kushiriki katika juhudi hii hadi mwisho wa enzi, na Yesu ameahidi kutotuacha kamwe tunapotii amri yake ya kufanya wanafunzi ulimwenguni pote. Malengo haya yameelezwa kwa uwazi katika kipengele cha Malengo ya Somo , na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote, wakati wa majadiliano na kipindi chote uwapo pamoja na wanafunzi. Kama ilivyoelezwa hapo awali, suala la kuwekea mkazo na kuzingatia daima malengo haya unapoendelea kupitia maudhui na vipengele vya somo hili ni lenye umuhimu mkubwa. Tunapozingatia malengo haya, tutatumia kila awamu ya ufundishaji wetu na taarifa zote zilizomo katika somo kuwasaidia wanafunzi wetu kuelewa malengo haya na kuyaweka ndani ya fahamu zao kwa lengo la kuwafundisha wengine. Tutavuna tunachopanda hapa. Kadiri unavyotumia muda mwingi kuelewa malengo na kuwaongoza wanafunzi wako kuyaelewa na kuyafikia, ndivyo matunda yako yatakavyokuwa bora kimahususi katika vipindi vyako vya ufundishaji, na kuhusiana na moduli za Capstone kwa ujumla.
1 Ukurasa 81 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online