Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 4 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
Ibada hii inakazia kutoa kipaumbele kwa maneno ya mwisho ya Yesu, na jinsi maneno hayo yanavyotuhimiza kuhubiri habari njema za wokovu na Ufalme wake hadi miisho ya dunia. Kanisa la Yesu Kristo limeagizwa na Mkuu wake kwenda kuhubiri Injili yake kwa watu wote wa dunia. Kwa maana hii Kanisa ni jumuiya iliyokombolewa na ni jumuiya ya ukombozi, sisi ni jumuiya iliyookolewa na pia jumuiya inayotangaza wokovu. Tumeona matunda na utajiri wa wokovu wa neema wa Mungu, na vile vile tumeitwa kwenda na kuwashirikisha wengine ahadi na tumaini la ukombozi katika Yesu Kristo. Lengo hapa liko wazi: tunapaswa kuhubiri Injili kwa kila kiumbe. Huu ni ushuhuda ulioje wa nia ya Mungu ya kuvuna kutoka katika kila koo, kikundi, kabila, taifa, lugha, na jamaa duniani watu ambao watakuwa wake na watakaomtumikia milele. Ni upendeleo wa ajabu jinsi gani tulio nao kutangaza habari hizi bila aibu, kwa ubunifu, nguvu, na unyofu wote ambao Roho wa Mungu anaweza kutupa, na kudhamiria, ndani kabisa ya mioyo yetu, kutokata tamaa hadi kazi hiyo ikamilike. Hakika, hili lilikuwa Neno lake la mwisho kwetu, na kwa ajili yetu sisi tulio Kanisa lake la kila kizazi kipya. Neno hili litabaki kuwa Neno la utume na uzima wetu, hadi atakapokuja. Mifano hii ya kujenga daraja inaangazia mambo muhimu, pengine la muhimu zaidi likiwa ni uchunguzi wa nini maana ya Mungu kumchagua mtu. Kuna maoni mengi yanayokinzana kuhusu jambo hili hasa linapohusishwa na tabia na utendaji wa Mungu. Ikiwa Mungu anaweza kumchagua mtu mmoja, je, hiyo inamaanisha kwamba anaweza pia kumkataa mwingine? Je, Mungu anawezaje kuchagua wakati Maandiko yanadokeza kwamba hakuna upendeleo kwa Mungu? Vipi kuhusu Mungu kutenda kwa udhalimu – je, Mungu hufanya maamuzi kiholela bila mpangilio, au ikiwa anafanya kwa makusudi, je, ametujulisha ni kigezo gani au sifa gani ambayo anaitumia anapofanya maamuzi? Maswali haya na yanayohusiana nayo ni ya msingi na yanaweza kujitokeza katika somo la uchaguzi la wiki hii. Usifadhaike kwa swali lolote kati ya haya; tunapaswa kushughulika na kila moja kwa nia iliyo wazi na tukiwa na Biblia zetu zilizofunguliwa, tukitafuta kwa kadri tuwezavyo kukabiliana na matokeo ya kila swali. Hata hivyo, hatupaswi kujifanya kana kwamba tunaweza kuzungumza juu ya nia ya ndani ya Mungu kwa uhakika kamili, hasa kuhusu vitu au masuala ambayo Yeye mwenyewe hajatufunulia mawazo yake juu ya mambo hayo. Kanuni nzuri ambayo kwayo tunapaswa kufanya kazi imo katika kifungu hiki muhimu katika Kumbukumbu la Torati:
2 Ukurasa 81 Ibada
3 Ukurasa 82 Kujenga Daraja
Made with FlippingBook - Share PDF online