Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 4 7

THEOLOJIA YA KANISA

Kumb. 29:29 - Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii. Unaposhughulika na dhana hizi ngumu pamoja na wanafunzi, fahamu tu kwamba si kila kitu ambacho Mungu anajua na kufikiria kimefunuliwa katika Maandiko, lakini kile ambacho ameweka wazi hutupatia ufahamu wa kutosha kabisa na mpana wa mapenzi yake, kiasi cha kuweza kutusaidia kutii mapenzi yake kwa shangwe. Hatupaswi kusisitiza kwa uhakika ambapo Mungu hajatupatia uhakika huo. Badala yake, tunapaswa kutakasa akili zetu, kulichunguza Neno, na kujisalimisha kwa uhalisia na ajabu ya fumbo la Mungu kuhusu masuala ambayo hayajafunuliwa kwa uwazi au hatuwezi kuyaelewa kikamilifu. Wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo, kama ambavyo Paulo anawaambia Wakorintho katika 1 Wakorintho 13. Unyenyekevu ungependekeza kwamba tujizuie kusisitiza kwa ujasiri kile ambacho hakijafundishwa ndani ya mipaka ya ufunuo. Zaburi 131 ni andiko kuu la mwanatheolojia na mwanafunzi wa Biblia mnyenyekevu. Zab. 131:1-3 - Bwana, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. 2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. 3 Ee Israeli, umtarajie Bwana, Tangu leo na hata milele. Uteuzi wa Mungu wa Yesu kama Masihi ni aina maalum ya uteuzi uliotajwa katika Maandiko, na katika akili yangu, hii ndiyo aina muhimu zaidi ya uteuzi. Kwa mfano, Maandiko yanataja kundi fulani la malaika walioteuliwa na Mungu, na andiko moja kimsingi linawataja kama “malaika wateule” (1 Tim. 5:21; taz. 1Kor. 6:3; 2 Pet. 2:4; Yuda 6). Pia, chaguo la Mungu la Daudi kuwa mtu ambaye kupitia kwake Masihi angekuja na kutawala ni muhimu sana katika suala la kusudi la Mungu la kuchagua (1 Sam. 16:7-12; rej. 2 Sam. 7:8-16). Bila shaka, Agano Jipya linazungumza kuhusu Yesu kuchagua wanafunzi na Mitume wake (Lk 6:13; Yoh. 6:70; 15:16; Mdo 9:15; 15:7). Haya yote, pamoja na mengine, yametajwa lakini hakuna yaliyo muhimu kama uteuzi wa Mungu wa Masihi, na ukombozi wetu na wokovu “katika yeye.” Kitabu cha Isaya kimejaa marejeo ya Mtumishi wa Mungu, na mara nyingi

 4 Ukurasa 83 Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Share PDF online