Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 4 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

kinamrejelea mtumishi huyu wa Bwana kama “mteule wangu” (ona Isa. 42:1; taz. Mt. 12:18). Katika Injili za sinoptiki au “Injili Ndugu” (yaani, Mathayo, Marko, na Luka), Luka peke yake ndiye anayemtaja Yesu kama Mteule (9:35; 23:35). Katika Waraka wa kwanza wa Petro, anamhusisha Yesu kwa uangalifu na rejea nyingine ya Isaya (Isaya 28:16 katika 1 Petro 1:20 na 2:4, 6, akizungumza kuhusu Yesu kama Jiwe la kujikwaa, teule lililochaguliwa katika Sayuni). Uteuzi wa Mungu wa Yesu ndilo wazo kuu la kitheolojia katika majadiliano yote ya Biblia kuhusu chaguo la Mungu, kwa kuwa kupitia tendo la kipekee na lisiloweza kurudiwa la Yesu kama Masihi wa Mungu na Mpatanishi wetu, Mungu anatekeleza kusudi lake la wokovu kupitia Kristo kwa ajili ya ulimwengu mzima. Kama utakavyoona, na unavyopaswa kukazia pamoja na wanafunzi, chaguo la Mungu kwa Yesu linatengeneza msingi na uwezekano wa uchaguzi wa Mungu kwetu ndani yake. Ni muhimu ukazie wakati wa kipindi hiki kwamba uchaguzi ni “uchaguzi katika Kristo”; unajumuisha kitendo cha Mungu cha kutukomboa kutoka katika utumwa wetu wa dhambi, hatia tunayopata kutokana na dhamiri yetu yenye dhambi, na ukombozi wa ajabu kutoka katika nguvu zake tunaopata kupitia imani katika Yesu Kristo. Maandiko ya msingi kama Waefeso 1:4-5, 11, na Warumi 8:29 yameweka wazi ukweli kwamba tumechaguliwa katika Kristo. Kwa namna fulani, haisaidii kufikiria uchaguzi wa watu binafsi kama msingi wa uchaguzi; Yesu sio tanbihi au mfano tu ambao Mungu anautumia kuonyesha chaguo lake kuu la wanadamu kwa ajili wokovu. Badala yake, uchaguzi unapaswa kuchukuliwa kuwa ndani ya Kristo na kwa njia ya Kristo. Uteuzi wa Mungu wa wanadamu kwa ajili ya wokovu hutokea katika nafsi ya Yesu. Yesu ni Mpatanishi wa wanadamu wote (1 Tim. 2:5-6), na wale ambao Mungu huwaita kwake wote hutubu na kumwamini Yesu Kristo hata kupata wokovu (1 Yoh. 5:11-13). Mungu anatuchagua katika Kristo, ambaye ndiye msingi wa yote ambayo Mungu anafanya katika suala la wokovu wa mwanadamu.

 5 Ukurasa 91 Kipengele namba II-B-3

Ingawa si muhimu kutumia muda mwingi juu ya mjadala wa muda mrefu wa kihistoria kuhusu fundisho la uchaguzi wa Mungu, ni muhimu kujua kwa muhtasari wa jumla baadhi ya mambo yahusuyo mjadala huu katika Kanisa kuhusu uchaguzi.

 6 Ukurasa 91 Kipengele namba II-C

Made with FlippingBook - Share PDF online