Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 4 9
THEOLOJIA YA KANISA
Kumekuwa na mvutano mwingi katika historia ya Kanisa juu ya maana kamili ya fundisho la kibiblia la uchaguzi. Migogoro muhimu zaidi pengine imetokea juu ya mawazo ya Kipelagia ( Pelagianism ya karne ya 5 na 6), na wakati wa kipindi cha Matengenezo. Msingi wa mabishano hayo ni hoja ya ikiwa sisi, kama wanadamu tulioanguka, tunao uhuru wa kumgeukia Mungu kwa ajili ya wokovu mbali na chaguo zuri la Mungu na upaji wa neema yake kwa njia ya Roho Mtakatifu, au tumepotoka sana katika hali yetu ya kupotea kiasi kwamba hatuna kabisa uhuru wa kuchagua au kukataa neema ya Mungu katika Kristo. Pelagianism ilielezea fundisho lake kwa njia hii: utashi wa wanadamu haujaharibika sana kiasi kwamba hatuwezi kuitikia amri ya Mungu ya kutubu na kuamini. Mtazamo huu ulichukuliwa na kueleweka kumaanisha kwamba watu binafsi wanaweza kukubalika na kuwa waadilifu bila kuchaguliwa na Mungu kwa njia ya neema yake kuu, na hawana haja ya kujihusisha kwake kupitia uchaguzi. Fundisho hili la uwezo wa kibinadamu lilikanushwa kwenye Baraza la Orange (529), ambalo pia lilikanusha aina ya “unusu-Pelagia,” ambayo ilifundisha kwamba wanadamu wanaweza kumchagua Kristo pasipo uhitaji wowote wa neema maalum ya Mungu. Wakati huo, Kanisa katika nchi za Magharibi lilishikilia maoni ya uchaguzi ambayo yalijengwa juu ya wazo la Augustine la “aina mbili za kuchaguliwa kabla” ( double predestination ). Fundisho hili lilifundisha kwamba Mungu alichagua wateule kwa ajili ya wokovu wake, na kwamba alichagua “waliokataliwa” (yaani, waliopotea na wasiookolewa) kwa ajili ya hukumu. Uchaguzi kama fundisho la wakati wa Matengenezo ya Kanisa ulifikiriwa upya na kufanyiwa marekebisho, na masuala yaliyotokana na mjadala huo yanaendelea kuchochea mivutano na migogoro hadi sasa. Wengi wa Wana-matengenezo wakuu walishikilia wazo la “uchaguzi usio na masharti” ( uncondintional election ), ambao leo umehusishwa moja kwa moja na kile kinachojulikana kama mtazamo wa “Ukalvini” wa uchaguzi. Mafundisho haya yalijengwa juu ya mtazamo wa Augustine, na kusisitiza kwamba uchaguzi wa Mungu wa watu binafsi ndio msingi na kigezo cha kila kitu kingine katika wokovu. Kile ambacho Mungu anafanya katika uchaguzi hakiamui tu hatua ya kwanza, bali kinaamua wokovu mzima wa wateule, ambao Mungu anauweka kwa chaguo lake mwenyewe na kuudumisha kulingana na mpango wake mwenyewe. Fundisho hili lilikazia azimio la Mungu kabla ya wakati kuhusu wale ambao wangepokea wokovu na pia wale waliowekwa
Made with FlippingBook - Share PDF online