Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 5 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
rasmi kwa ajili ya hukumu. Uteuzi wa Mungu wa wateule uliegemezwa juu ya rehema yake pekee na bila kurejelea sifa au thamani ya wateule. Mwitikio mkubwa kwa mafundisho haya ulikuja katika mfumo wa mapokeo ambayo leo yanajulikana kama “Uaminiani” ( Arminianism ). Uaminiani ulilenga hasa wazo la kukataa maoni ya uchaguzi usio na masharti. Badala yake, mapokeo haya yalifundisha kwamba uchaguzi kwa namna fulani ulikuwa “wenye masharti,” yaani, Mungu alichagua wale aliowaona tangu mwanzo kwamba wangeitikia Injili kupitia wito wa jumla wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya wokovu. Mtazamo wao unazingatia uhuru wa mwanadamu na neema ya Mungu inayotolewa kwa kiasi fulani kwa wanadamu wote, ambayo inaturuhusu kuitikia zawadi ya bure ya Mungu ya neema. Kinachojulikana kama “Hoja Tano za Ukalvini” (TULIP) ni muhtasari mzuri wa msimamo wa Wakalvini, na njia kuu ya kutambua tofauti kati ya Ukalvini na Uaminiani. Hoja hizi ni pamoja na wazo la upotovu kamili, uchaguzi usio na masharti, upatanisho mdogo (au wenye mipaka), neema isiyozuilika, na uvumilivu wa watakatifu. Leo, kuna dhana nyingine mbadala katika majadiliano ya kitheolojia kuhusu uchaguzi usio na masharti, inaitwa “falsafa ya kilimwengu” ( Universalism ). Mtazamo huu, ambao ni wa kawaida katika duru za kiliberali, unadai kwamba wanadamu wote walijumuishwa katika kazi ya wokovu ya Mungu katika Yesu Kristo. Kwa hiyo wanadamu wote ni wateule wa Mungu, na hatimaye, wanadamu wote wataokolewa mwishoni. Labda mtazamo unaojadiliwa zaidi kuhusiana na suala hili katika duru za kitheolojia unahusiana na theolojia ya uchaguzi ya Karl Barth. Barth alitoa maoni ambayo yalidai kwamba uchaguzi kutoka kwa Mungu kimsingi ni wa Kristo (wenye kiini chake katika Yesu Kristo). Mungu hachagui kikundi cha watu binafsi bali amemchagua Kristo mwenyewe. Yeye pekee ndiye mteule, na, sambamba na hilo, Kristo ndiye pekee ambaye Mungu alimkataa. Juu ya Kristo ilianguka shutuma na kukataliwa, na sasa kupitia kazi yake, uchaguzi unawaangukia wanadamu wote.
Ni muhimu kutambua kwamba mwelekeo wowote wa kimtazamo ambao mtu atachukua kuhusiana na uchaguzi, dhana iliyo wazi ni kwamba Mungu hachagui kwa msingi wa kazi za kibinadamu (Rum. 9:11). Kulingana na Waefeso 1:4 5, tumechaguliwa na Mungu kuwa watakatifu na wasio na hatia mbele zake,
7 Ukurasa 91 Kipengele namba II-C-1
Made with FlippingBook - Share PDF online