Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 5 1
THEOLOJIA YA KANISA
tuliofanywa wana kwa njia ya Yesu Kristo. Si kwa kadiri ya juhudi zetu au mapenzi yetu, bali ni kwa damu ya Yesu Kristo na sawasawa na uradhi wa mapenzi yake (Efe. 1:7; Yoh. 1:12-13).
Tafadhali sisitiza kwa wanafunzi wako kwamba uchaguzi wa Mungu haufanyi umisheni na uinjilisti kukosa ulazima, badala yake, uchaguzi wa Mungu unathibitisha kwamba umisheni na uinjilisti ni kazi ya lazima. Suala la Mungu kutuhakikishia kwamba wale wanaotubu na kuamini wataokolewa halibatilishi wajibu wetu wa kuuambia ulimwengu kuhusu Yesu na upendo wake. Uchaguzi wa Mungu haujumuishi tu wokovu wa watu wa Mungu, bali unajumuisha pia njia ambazo kupitia hizo watu hao wanaokolewa. Uchaguzi wa Mungu kwa waliookolewa katika Yesu Kristo unamaanisha kwamba wamesikia habari njema ya Injili, na kuitikia Injili kwa toba na imani. Tunaokolewa kupitia kazi ya utakaso ya Roho Mtakatifu na kupitia imani katika kweli ya Injili; lazima tusikie na kuamini ili tupate kuokolewa (2 Thes. 2:13). Kutokana na andiko hili na maandiko mengine mengi, ni wazi kwamba mahubiri na mafundisho ya kweli ya Kristo ni muhimu kwa wokovu, na kwa ajili ya kutengeneza msingi kwa ajili ya wito wa Mungu wa uchaguzi (Rum. 10:14-17; rej. Mdo. 18:9-11). Mojawapo ya masuala muhimu yanayohusu fundisho la uchaguzi (pamoja na wazo dada la “kukataliwa,” au tendo la Mungu kuwatupa wale ambao hawajachaguliwa) ni kama au la uchaguzi wa Mungu ni wa ushirika na wa jumuiya, wa mtu binafsi na wa kibinafsi, au aina fulani ya uchaguzi wa mseto kati ya dhana hizo mbili. Tunasisitiza kote katika somo hili kwamba tumechaguliwa katika Kristo, na kwamba namna hii ya kuchaguliwa kwa vitendo na kiroho ndiyo kiini cha fundisho hili. Maandiko katika Agano Jipya yanaunga mkono madai ya pande zote mbili, kwamba uchaguzi una kipengele cha mtu binafsi na pia kipengele cha jumuiya. Kwa mfano, maelezo ya wazi ya Waefeso yanadokeza kwamba uchaguzi kwa namna fulani ni wa jumuiya, kama inavyoonyeshwa na matumizi ya Paulo ya neno “sisi” (1:4-5, 12). Zaidi ya hayo, katika mojawapo ya maandiko yaliyonukuliwa mara nyingi katika rejea hapa, Warumi 8:28-30, Paulo anatumia viwakilishi vya wingi, “wale,” ambao Mungu aliwajua tangu asili, ndio aliowachagua tangu asili,
8 Ukurasa 94 Kipengele namba III-C
9 Ukurasa 94 Kipengele namba III-D
Made with FlippingBook - Share PDF online