Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 5 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

akawaita, akawahesabia haki, na kuwatukuza. Tena, Warumi 9 inazungumzia fundisho la uchaguzi kwa mujibu wa uchaguzi wa Israeli, na uchaguzi wa kibinafsi kama kipengele ndani yake. Kauli hii ya Paulo, hata hivyo, inalinganishwa na kauli yake katika Warumi 9:8 ambapo anaonyesha kwamba “si wote walio wazao wa Israeli ni Israeli” (9:6, 8), na kisha kwa ustadi anajenga hoja ya jambo hilo katika mfano mmoja wa Yakobo na Esau (9:7, 11-13). Wale wanaowekea mkazo zaidi katika dhana ya uchaguzi wa mtu binafsi wanasimamia mistari kadhaa, ikiwa ni pamoja na maandiko kama vile Yohana 6:37-40; 10:14-16, 26-29; 17:2, 6, 9, 24. Kwa faida ya somo letu, tunasisitiza haja ya kuzingatia mada ya uchaguzi katika msingi wa tendo la Mungu kumchagua kwa Kristo, na kuchaguliwa kwetu katika Kristo. Katika maswali haya, utaona kuwa lengo ni kuzingatia zaidi maudhui na kweli zinazohusishwa na maarifa yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza ya video. Fundisho la uchaguzi ni dhana muhimu inayohusiana na Kanisa, na inawezekana kukengeushwa na mijadala mingi inayoonekana kuwa muhimu na inayohusiana dhana hii. Jambo kubwa katika mjadala huu ni kuangazia jinsi wanafunzi wanavyoelewa dhana ya uchaguzi wa Mungu katika Kristo , kwa maana kwamba Mungu ametekeleza uchaguzi wake kwetu katika Yesu Kristo. Zingatia wazo hili, na utafute kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa majibu kulingana na wazo hili muhimu, pamoja na malengo mengine ya somo katika sehemu hii ya kwanza. Agizo Kuu linatumika kama kiini cha agizo la kibiblia la Yesu kwa Kanisa kuhubiri habari njema za wokovu wake kwa ulimwengu mzima, na kufanya wanafunzi wake kila mahali. Agizo hili la kwenda kufanya wanafunzi wa Yesu kati ya vikundi vyote vya watu wa dunia limesisitizwa kiunabii katika Agano la Kale (Isa. 45:22; taz. Mwa. 12:3) na limetimilizwa na kuthibitishwa tena katika Agano Jipya (Mt. 9:37-38; 28:19; Mdo 1:8). Kiini cha kufanya wanafunzi ni kuwaeleza wazi wazi wale ambao hawajapata kusikia hadithi ya Yesu wa Nazareti, ikijumuisha ukweli kuhusu maisha yake, huduma na mateso yake, lakini hasa ukweli na maana ya kusulubishwa kwake pale Kalvari kama tendo la fidia ya dhambi na ushindi dhidi ya shetani (1Kor. 15:3; Kol. 2:14-15). Tangazo hili la Injili pia linajumuisha ushuhuda kuhusu ufufuo wa Kristo kutoka katika wafu, kupaa kwake mbinguni

 10 Ukurasa 95 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 11 Ukurasa 97

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook - Share PDF online