Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 5 3
THEOLOJIA YA KANISA
kwenye mkono wa kuume wa Mungu (Lk 24:46-48; Rum. 4:25; 1 Kor. 15:3-4; Efe. 1:20-23), na tumaini la utimilifu wa kazi yake katika Parousia au Ujio wa Pili wa Yesu Kristo (Mdo. 3:19-21). Katika kuwafundisha wanafunzi wako, fafanua kwa uwazi kwamba nia ya msingi ya amri ya Kristo kwa ajili ya utume ni upendo unaobidisha ambao Kristo ameufunua kupitia matendo yake kwa ajili yetu (2 Kor. 5:14-21). Siri na kina cha Umwilisho vinafunua ajabu na upeo wa upendo wa Mungu kwa wanadamu (Yoh. 3:16). Katika kutangaza Habari Njema, wale wanaotangaza Habari Njema wamebidishwa, wamedhamiria, wanatawaliwa na wingi wa upendo wa Mungu katika Kristo. Yesu kama Mwana wa Mungu, Mwanzilishi wa uzima (Mdo. 3:15) na Bwana wa utukufu (1 Kor. 2:8), sasa amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Ni Bwana huyu aliyefufuka na kushinda ambaye analiamuru Kanisa lake kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wake (Mt. 28:18-19). Kwa maana halisi, kufanya wanafunzi kwa kutii Agizo Kuu ni kuendeleza tu kazi ambayo Kristo mwenyewe alianzisha kupitia kutangaza kwake Ufalme duniani. Ni ushuhuda wa mitume kwamba Yesu alikwenda huku na huko akizishinda kazi za shetani na kutenda mema (Mdo 10:38), akitangaza ujio wa Ufalme wa Mungu (Mk. 1:14-15), na kuja kutafuta na kuokoa wale waliopotea, wale ambao walihitaji kupata neema ya Mungu iokoayo, ambayo inapatikana ndani yake pekee (Lk 19:10). Itakuwa muhimu kusisitiza kuhusu asili ya tume, yaani, vipengele mbalimbali vya Agizo na jinsi vinavyohusiana na utii wetu kwa Agizo hilo. Habari Njema za Kristo zinapaswa kuunganishwa na kazi ya kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Yesu. Tunapaswa kufanya wafuasi wa Kristo kati ya mataifa yote, kuanzia Yerusalemu na Uyahudi, kuendelea hadi Samaria iliyo karibu, na hatimaye kwenda miisho ya nchi (Lk 24:47-48; Mdo. 1:8). Tabaka zote na makabila ya watu yanapaswa kulengwa katika juhudi zetu, wakiwemo Wayahudi (Mdo. 2:5-11) na mataifa (Mdo. 13:46; Rum. 1:16). Roho Mtakatifu wa Mungu atatupatia uwezo wa kufanya kazi hii: yeye ndiye anayeuhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu (Yoh. 16:8-11), ndiye anayeangazia akili na fahamu za wale wanaosikia kweli ya Yesu Kristo (1 Kor. 2:9-15), na kuifanya upya nafsi ya mtu kupitia maisha ya Kristo mwenyewe (Tito 3:5). Tunapaswa kushiriki katika juhudi hii mpaka wote wamesikia, hata siku ya kuja kwake Kristo (Mt. 24:14).
Made with FlippingBook - Share PDF online