Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 5 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

Katika kufanya marudio ya dhana za somo hili, ni muhimu kwamba ujikite kwenye malengo ya somo. Kwa namna fulani, upana wa mada zinazoshughulikiwa katika somo hili unakulazimu kwamba uzingatie kwa makini malengo ya somo ili usivutwe kupita kiasi nje ya masuala muhimu. Ingawa hupaswi kusita kujadili kwa kina maswali kadha wa kadha ambayo wanafunzi wako wanaweza kuwa nayo kuhusu dhana ambazo ni ngumu kuelewa, unahitaji kuhakikisha kuwa wamepata uelewa wa jumla wa dhana zilizo hapa chini. Hasa hasa zingatia uhusiano kati ya fundisho la uchaguzi na jukumu letu la kufanya wanafunzi ulimwenguni kote kwa kutii Agizo Kuu. Kwa kadiri iwezekanavyo, wawezeshe wanafunzi kuelewa uwiano kati ya mada hizo. Huku ukizingatia mada za jumla, katika sehemu hii ya maswali zingatia kimahususi maswali na wasiwasi wa wanafunzi. Bila shaka, maswali mengi yanaweza kuibuka kutokana na mjadala juu ya tofauti katika hoja za mafundisho ya uchaguzi, kwa sababu hiyo, jiandae kuruhusu muda wa kutosha ili kushughulikia athari mbalimbali za mitazamo na tofauti hizo. Hasa katika fundisho la uchaguzi, kuna masuala kadhaa ambayo yanahitaji kutafakari na kujadiliana kwa kina, na baadhi ya masuala husika yanaweza kusababisha viwango tofauti vya mivutano. Ni muhimu kusisitiza jukumu la mambo ya siri ya Mungu na ukomo wa ufahamu wetu katika elimu yoyote ya kitheolojia. Mungu ametupatia elimu ambayo ina mambo mengi na inapita ufahamu wetu, lakini hajatupatia ufahamu wa kuweza kuelewa kila kitu. Tunahitaji kuwa wanyenyekevu vya kutosha ili kukubali kwamba kuna mipaka halisi katika uelewa wetu wa nia na mapenzi ya Mungu, na tunapaswa kuwa waangalifu katika madai yetu kuhusu kile ambacho Mungu anajua kwa ukamilifu wote. Kupitia majibu yako na mwenendo wako, toa kielelezo kwa wanafunzi wako kuhusu maana ya kuwa salama katika kuyapokea mambo ya siri ya Mungu kama yalivyo. Mambo yaliyofunuliwa ni yetu na yaliyofichwa ni ya Bwana (Kum. 29:29). Makosa yetu mengi katika kukisia kisia tafsiri za masuala ya kitheolojia mara nyingi hutokana na kiburi chetu cha kudhani kwamba tunaweza kujua kila kitu kuhusu Mungu na kazi zake ulimwenguni. Hatuwezi! Kwa sababu hiyo, tunapaswa kushughulika na maswali yetu kwa unyenyekevu na uwazi. Roho Mtakatifu ndiye mwalimu wetu na tunaweza kumtegemea tunapoendelea na masomo yetu pamoja (1 Yoh. 2:27).

 12 Ukurasa 107 Muhtasari wa Dhana Muhimu

 13 Ukurasa 108 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

Made with FlippingBook - Share PDF online