Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 5 5
THEOLOJIA YA KANISA
Mifano hii imeundwa ili kuwawezesha wanafunzi kutumia kweli hii ngumu, ambayo hata hivyo ni yenye kuburudisha kuhusu uchaguzi na Agizo katika hali halisi za maisha. Ni muhimu kujua kwamba katika hali nyingi, tunapotumia Neno la Mungu, mara nyingi kuna nyakati ambapo hata tafakuri zetu zilizo bora zaidi na hata yale mawazo ambayo ni ya kibiblia zaidi hayatatoa majibu rahisi kwa mambo tusiyoweza kuyaelewa. Tunachotafuta hapa ni uwazi na umakini katika kutafuta kuelewa ukweli wa hali au jambo husika kwa uangalifu, na kuhusianisha Neno la Mungu na hali au jambo hilo kwa kutumia hekima na busara kadri iwezekanavyo. Huenda kukawa na zaidi ya jibu moja sahihi katika hali au jambo fulani, na ni lazima tuwasaidie wanafunzi wetu kuwa wa kibiblia bila kuwa wenye kuhukumu mambo pasipo maarifa, au wenye misimamo migumu ya kidini ambayo haina uzima wa Mungu ndani yake. Ili kuwa wanafunzi wazuri wa Maandiko, wanafunzi wetu lazima waweze “kutumia kwa halali neno la kweli” (2 Tim. 2:15), na kufanya aina ya uchambuzi ulio mzuri na muhimu unaohitajika katika visa hivi. Katika mijadala yako kuhusu mifano hii halisi, wasaidie wanafunzi wako kuitazama kutoka kila upande kimtazamo ili kugundua majawabu bora zaidi ndani ya visa husika. Si jambo gumu kuona upana wa matumizi ya somo yanayoweza kufanyika hapa, lakini njia mojawapo muhimu ya kuhusianisha somo hili na huduma halisi ni ukuu wa Mungu katika uchaguzi na utume (umisheni). Mungu wetu ndiye anayetawala, Yesu Kristo ndiye Bwana wa wote, na tunaweza kujua kwamba hakuna kamwe kitu chochote tunachoweza kukabilina nacho kwa njia yoyote ambacho Mungu wetu hana uwezo wa kutupatia ujuzi na nguvu zinazohitajika ili kutimiza mapenzi yake. Sisitiza ukweli huu mkuu unapowasaidia wanafunzi kuhusianisha kweli za somo hili na maisha na huduma zao za kibinafsi. Unapaswa kuwa umezungumza vyema na wanafunzi kuhusu muda ambao wanatakiwa kufanya na kukabidhi kazi zao hivi karibuni. Kwa mfano, kufikia mwisho wa somo la pili, unapaswa kuwa umewaeleza wanafunzi hitaji la wao kuwa wamefikiria na kufanya kazi ya msingi kwa ajili ya Kazi ya Huduma kwa Vitendo. Sasa, kufikia mwisho wa somo la tatu, unapaswa pia kuwa umesisitiza haja ya wao kuchagua kifungu kwa ajili ya Kazi yao ya Uchambuzi wa Maandiko (eksejesia).
14 Ukurasa 109 Mifano Halisi
15 Ukurasa 111 Kuhusianisha Somo na Huduma
16 Ukurasa 113 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online