Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 5 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
Kazi hizi zote mbili zina kawaida ya kuwashitukiza wanafunzi mwishoni mwa kozi, kwa hiyo hakikisha unawasisitiza kuhusu kazi zinazopaswa kufanywa, viwango vya kuzingatia wanapozifanya, na tarehe ambayo kazi zinatarajiwa kukamilika. Wape taarifa stahiki kuhusu kazi zao za mwisho na kazi nyingine zozote husika, na uwasihi wajipange na kuwa tayari kwa kazi hiyo kubwa iliyo mbele yao. Usiache kusisitiza mambo haya kwa wanafunzi wako kwani, katika masomo yoyote, mwisho wa kozi unashughuli nyingi, huku mambo mengi yakitarajiwa na wanafunzi huhisi shinikizo la kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ili kuendana na tarehe za kukamilisha mambo yote. Njia yoyote ambayo unaweza kutumia kuwakumbusha juu ya hitaji la kujipanga mapema itakuwa ya manufaa kwao, kwamba watalitambua hilo mara moja au la. Kwa sababu hii, tunashauri kwamba ufikirie kukata maksi kadhaa kwenye kazi zitakazokusanywa kwa kuchelewa. Ingawa kiwango cha maksi za kukatwa kinaweza kuwa cha kawaida, utekelezaji wako wa kanuni ulizojiwekea utawasaidia kujifunza kuwa makini, wenye ufanisi na kujali muda wakati wanapoendelea na masomo yao.
Made with FlippingBook - Share PDF online