Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 5 7

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa katika Kazi

MAELEZO YA MKUFUNZI 4

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 4, Kanisa katika Kazi . Lengo la jumla la somo hili katika moduli hii ya mtaala wa Capstone iitwayo “Theolojia ya Kanisa” ni kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa kwa uwazi na kuweza kuelezea kwa wengine mitazamo na vipengele mbalimbali vya Kanisa, kueleza jinsi tunavyoweza kugundua jumuiya halisi ya Kikristo kupitia matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. Tutakuwa tukiangalia utambulisho na kazi za Kanisa kupitia sifa zinazotolewa katika Kanuni ya Imani ya Nikea, mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa, na kanuni ya Mt. Vincent. Kupitia vyanzo hivi tunaweza kuelewa na kutathmini mapokeo na mafundisho yanayojidai kuzungumza kuhusu asili ya Kanisa na mafundisho ya Kikristo. Pia tutachunguza tabia ya kazi za Kanisa ulimwenguni kwa kuchunguza taswira au lugha za picha mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya. Kupitia tafsiri ya mifano kama nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu, Kanisa kama ubalozi na wakala wa Ufalme wa Mungu, na Kanisa kama jeshi la Mungu, tutaelewa kile ambacho Kanisa limeitwa kuwa na kufanya ulimwenguni. Kama ilivyokuwa katika uongozi wako wa masomo yaliyotangulia, kumbuka tena jinsi ilivyo muhimu kuelekeza kipindi cha darasa lako kwenye malengo ya kujifunza ya somo hili. Wajibu wako kama mshauri ni kusisitiza mawazo yanajitokeza kupitia malengo kwa njia ambayo yatakufanya uwe na shabaha na malengo yaliyo wazi kwako katika kipindi chote cha somo. Sisitiza malengo wakati wote, lakini hasa wakati wa mijadala na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo haya katika kipindi chote cha somo, ndivyo nafasi zinavyokuwa nzuri zaidi kwa wanafunzi wako kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Ibada hii inaangazia fursa ambayo Kanisa linayo katika kuwakilisha Ufalme unaokuja hivi karibuni wa Bwana wetu Yesu katika kile linachofanya na kusema ulimwenguni. Yesu anatuamuru sisi kwamba nuru zetu ziangaze, kibinafsi na kama jumuiya, kiasi kwamba matendo yetu yanapotazamwa na jirani zetu, waweze kumtukuza Mungu Baba aliye mbinguni kupitia matendo yetu (Mt. 5:14-16). Kumwakilisha mwingine ni kuungamanisha sifa zake na matendo yako, kumlazimisha aonekane katika mwanga wa kile unachofanya (au kushindwa kufanya).

 1 Ukurasa 117 Utangulizi wa Somo

 2 Ukurasa 117 Ibada

Made with FlippingBook - Share PDF online