Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 5 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
Kama mawakala na wawakilishi wa Kristo, tunamfunua kupitia kile tunachofanya, jinsi tunavyoenenda katika ulimwengu, na jinsi tunavyotenda kazi katika enzi hii. Wasaidie wanafunzi kutambua vyema nafasi ya ajabu waliyo nayo, kama watu binafsi na washirika wa makusanyiko, ya kuakisi, kama mwezi, miale tukufu ya Mwana wa Mungu. Ili kutimiza agizo hili, ni lazima walifahamu, na pia kulikumbatia. Hatua za kwanza ni kukaribisha changamoto na fursa ya kumwakilisha mbele ya wengine. Mojawapo ya ishara za enzi hii ya sasa ni kuenea na kukua kwa vikundi vya madhehebu na dini za uongo. Ni muhimu kwa wanafunzi katika jiji kuweza kutambua, kuelewa, na kukanusha mafundisho na mazoea ya vikundi vya kidini vya uongo. Kukata tamaa na ugumu wa maisha ya mijini kunaweza kuwafanya watu wa mjini wawe rahisi kuathiriwa na makundi yanayowawinda maskini na wanyonge. Katika mifano ya kujenga daraja ifuatayo unaweza kuona msisitizo wa kutambua ni nani walio wa kweli miongoni mwa wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo na wawakilishi wake. Ni muhimu kwa wanafunzi kuhamasishwa sana kujua vipengele na sifa mbalimbali za Kanisa la kweli, kile linachoamini na kufanya, ili kugundua makundi ya uongo na yasiyoakisi kielelezo sahihi na halisi cha Kanisa katika mitaa yao. Tafadhali, katika eneo hili, sisitiza kwa wanafunzi wako katika mjadala wako mfupi kwamba viongozi wa Kikristo lazima wawe na uwezo wa kujenga hoja zenye nguvu na kutetea imani halisi ya kihistoria dhidi ya mashambulizi. Si makanisa yote yanayodai kumwakilisha Kristo na Ufalme wake yaliyo halali; jukumu la wanafunzi, kama viongozi wanaoandaliwa, ni kuweza kusaidia makusanyiko yao kukua zaidi na zaidi katika maono ya Mungu kwa Kanisa lake, ili sisi sote tukue kufikia ukomavu kamili katika Yesu Kristo (Efe. 4:9-15; 2 Pet. 3:18). Kwa kuzingatia kuenea kwa migawanyiko na machafuko kati ya makanisa leo, umoja wa Kanisa ni mada muhimu ambayo tunapaswa kusisitiza katika ukuzaji wa uongozi wa Kikristo. Kama mitume wengine wote, Paulo anaonya makusanyiko ya kwanza ya Kikristo dhidi ya majaribu ya mafarakano, migawanyiko, na migogoro katika 1 Wakorintho 1:10-30, na kuwahimiza kuungamanishwa pamoja katika imani, utume, na ushirika. Katika maelezo yake ya kina juu ya mwili wa
3 Ukurasa 119 Kujenga Daraja
4 Ukurasa 121
Kipengele namba I-A
Made with FlippingBook - Share PDF online