Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 5 9

THEOLOJIA YA KANISA

Kristo, Paulo anasisitiza katika 1 Wakorintho 12 kwamba Roho Mtakatifu huwapatia washirika wa Kanisa, madhihirisho mbalimbali ya neema ya Mungu, lakini anafanya hivyo ili kuwepo na utendaji wenye uwiano na kiwango sawa cha huduma na upendo baina ya waamini wote. Kwa maneno mengine, kuna viungo vingi katika mwili wa Kristo, lakini mwili ni mmoja tu (rej. Rum. 12:3-8). Bila kujali Wakristo ambao wameamini katika nyakati zote katika sehemu mbalimbali, Yesu anasema kwamba kwa pamoja waamini wana mchungaji mmoja na kundi moja (Yoh. 10:16), tena katika sala yake ya ukuhani mkuu wakati wa mateso yake anaomba wazi wazi kwa ajili ya umoja wetu (17:20-26). Katika Wakolosai 3:11 na Wagalatia 3:27-28 tunaona kwamba Kanisa halijulikani kwa makundi; watu wote wanaomwamini Yesu Kristo wamekuwa wamoja, na hakuna aliye wa tofauti kwa msingi wa jinsia, rangi, kabila, hadhi ya kijamii, au historia. Kuwa wamoja katika Kristo kwa imani, hata hivyo, haimaanishi kwamba waamini watafanana kabisa katika kila eneo. Mtaguso wa Yerusalemu katika Matendo 15 unathibitisha kwamba imani ya Kikristo haihitaji kuweka watu katika utumwa wa mapokeo ya Kiyahudi au hisia za Mataifa. Makanisa hukusanyika kulingana na maeneo, kulingana na lugha na tamaduni tofauti. Tangu mwanzo, makanisa (makusanyiko) yamekuwa na tabia zao wenyewe, ibada za aina yao, fursa za utume, mateso na hatari, na usemi wa aina yao. Tunashikilia leo changamoto ile ile ambayo makanisa yamehisi katika nyakati zote: waamini wanapaswa kuishi pamoja kwa upendo na umoja kwa habari ya kiini cha imani yetu katika Kristo, bila kudai kwamba makusanyiko yote yaige mifumo yetu ya ibada, utume, mafundisho, na muundo. Tafadhali sisitiza kwa wanafunzi wako kwamba chaguo la Mungu la kuchagua washirika wake linajumuisha matawi yote ya Mzabibu, ambayo Yesu mwenyewe ndiye Shina letu sisi sote (Yoh. 15:4-5). Ingawa kila kusanyiko la Kikristo linaweza kuwa na changamoto zake za migawanyiko, mivutano, au migogoro, Mungu huwaita watu wake kuwa ni watakatifu. Jinsi gani? Lugha ya kibiblia kuhusu utakatifu inahusiana moja kwa moja na tabia halisi ya utakatifu ambayo tunatafuta kudhihirisha katika usafi wetu kibinafsi na katika ushirika (k.m., 1 Thes. 4:1-8). Lakini, pia lugha hiyo inarejelea hali au hadhi ya kutengwa na unajisi, na uovu, na wasio wa Mungu ili kutengwa kuwa milki ya Mungu, raha ya Mungu, na kwa ajili ya kusudi la Mungu. Ukweli kwamba Kanisa ni takatifu, basi, haimaanishi kwamba Kanisa (wala makanisa na

 5 Ukurasa 122

Kipengele namba I-B

Made with FlippingBook - Share PDF online