Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 6 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

makusanyiko yote yanayounda Kanisa) haliwezi kuguswa na aina yoyote ya dhambi au uchafu. Badala yake, inamaanisha kwamba Kanisa, kupitia kusudi la uchaguzi wa Mungu mwenyewe, limetengwa kuwa milki yake na kwa ajili ya matumizi yake, na kwamba linapaswa kutafuta kuwa kile ambacho limekusudiwa kuwa na kufanya kile ambacho limeitiwa kupitia wito wa Mungu. Hili linaendana kabisa na kuthibitishwa na kile ambacho Paulo anaonyesha katika mjadala wake kuhusu shauku yake ya kumtukuza Mungu katika Wafilipi 3:12, ambapo anasema kwamba kwa sasa, hakuwa mkamilifu bado na hakuwa ameufikia mwito mkuu wa Mungu katika Kristo. Hata kusanyiko la Korintho linaitwa takatifu, na washirika wake ni “watakatifu” (rej. 1Kor. 1:2). Sisi kama makusanyiko ni watakatifu, angalau kwa maana ya kwamba tumetengwa na Mungu kuwa milki yake, raha yake, na kwa ajili ya matumizi yake (2 Thes. 2:13; Kol. 3:12, nk.). Kwa kutumia neno “katoliki,” hatumaanishi kwamba muundo na mfumo wa Kanisa Katoliki la Roma ni sahihi na wenye mamlaka, au hata wa msingi. Tunachomaanisha hapa, hata hivyo, ni kwamba Kanisa linajumuisha wote wanaoamini, walio hai, waliokufa, na ambao bado hawajazaliwa, ambao wanaunda jumuiya moja ya Mungu ya mataifa yote, ya zama zote, ya ulimwengu mzima. Neno lenyewe linatokana na neno la Kilatini catholicus , neno linalohusiana na neno la Kiyunani katholikos ambalo linamaanisha “ulimwengu wote.” Wazo hilo linaonekana kuwa la kibiblia, ingawa viunganishi vya maneno haya halisi havijatajwa popote katika Agano Jipya. Njia rahisi ya kuelewa dhana ya ukatoliki wa Kanisa ni kufikiri kwa namna ya Kanisa zima au watu wote wa Mungu, wa nyakati zote, zama zote, koo zote, kabila zote, lugha zote, nchi na lugha zote. Neno hilo pia linaakisi sawasawa umoja wa Kanisa, ambao una maana kwamba tuna kusudi moja, utambulisho mmoja, utume mmoja, na hatima moja katika aina zote na miundo mbalimbali ambayo inawakilisha Kanisa moja la kweli. Itakuwa muhimu katika uwasilishaji wako wa somo hili kuchunguza baadhi ya matokeo ya ukweli huu, ambayo ni kusema kwamba kila muungano wa makanisa (dhehebu) ambayo yanamkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi na kuishi kulingana na ukiri huo, lazima utazamwe kuwa ni muungano au dhehebu sawa na mengine. Kwa sababu hiyo, hakuna sehemu, sekta, enzi, au dhehebu la Kanisa linayopaswa kujiona kuwa muhimu na bora zaidi au lenye mamlaka kuliko dhehebu lingine. Kwa hiyo, makanisa ya mijini yanapaswa kujitahidi kuchukua nafasi yake maalum

 6 Ukurasa 122

Kipengele namba I-C

Made with FlippingBook - Share PDF online