Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 6 1

THEOLOJIA YA KANISA

katika kuwashawishi wengine kwa ajili ya Kristo. Ukristo wa mijini hauhitaji kuwa tegemezi kupita kiasi au kutishwa na aina nyinginezo za ukristo au madhehebu, kwa kuwa wao ni sehemu ya Kanisa moja la kweli, katoliki (yaani, la ulimwengu wote).

Dhana kwamba Kanisa ni la kitume imejengwa juu ya ukweli kwamba imani na matendo ya Kanisa vimejengwa juu ya msingi wa ushuhuda na mafundisho ya mitume. Mtume Paulo anafundisha jambo hili wazi wazi katika waraka wake kwa Waefeso: Waefeso 2:19-22 – Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. 22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. Mitume wanayo nafasi ya juu na ya heshima kubwa katika historia na maendeleo ya Kanisa kwa sababu ya ushuhuda wao wa macho juu ya Yesu Kristo na kazi yake, hasa ufufuo wake, pamoja na ufunuo wao wenye mamlaka juu ya maana ya maisha na huduma ya Yesu kwa wanadamu na Kanisa. Kwa maana moja, mitume wamekuwa kigezo cha muono mzima wa Kanisa: maoni yao yanaunda msingi wa kuthibitishwa kwa kanoni ya maandiko ya Agano Jipya, uhalali wa uongozi na mafundisho ya Kanisa, na msingi wa kanuni zinazothibitisha uhalali wetu kama waamini wa kweli. Kuwakataa mitume ni kumkana Kristo; kwa sababu hiyo, Kanisa ni la kitume katika msingi wake. Sakramenti inaweza kufafanuliwa kama ibada au sherehe, iwe ilianzishwa na Yesu Kristo au kupitia historia ya Kanisa, ambayo inaeleweka kuwa njia ya neema au ukumbusho au ishara ya imani na matendo ya Kikristo. Kwa waamini wengine, hasa Waprotestanti, neno “sakramenti” linatumika tu kwa ajili ya taratibu na sherehe zilizoanzishwa na Yesu Kristo mwenyewe na si vinginevyo. Mambo mawili yanayotambuliwa na mapokeo yote ya Kanisa ni ubatizo na Meza ya

 7 Ukurasa 123

Kipengele namba I-D

 8 Ukurasa 125 Kipengele namba II-B

Made with FlippingBook - Share PDF online