Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 6 2 /
THEOLOJIA YA KANISA
Bwana. Sakramenti hizi mbili zimetajwa katika Agano Jipya na Yesu, na zote mbili zilishikilia nafasi na kipaumbele muhimu katika maisha na jamii ya waamini wa kwanza (Mdo 2:41-42; 10:47; 20:7, 11). Japokuwa Kanisa Katoliki na mapokeo mengine yamepanua wigo wa sakramenti kujumuisha idadi kubwa ya ibada na sherehe, ubatizo na Meza ya Bwana vinahusiana moja kwa moja na Yesu Kristo na kazi yake, hasa kuhusiana na kifo na ufufuo wake, na kuja kwake tena (Mt. 28:19-20; Mdo. 2:38; Rum. 6:3-5; 1 Kor. 11:23-27; Kol. 2:11-12). Maswali haya yameundwa ili kuangazia mambo makuu yanayohusiana na sehemu ya kwanza ya video. Kwa mara nyingine tena, tunatumia vigezo mbalimbali vya Kanuni ya Imani ya Nikea, mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa, na Kanuni ya Vicent ili kutambua vigezo gani vya Kanisa la kweli vyenye ufanisi zaidi na vyenye kusadikisha kibiblia. Unapojadili vigezo hivi, hakikisha kwamba unafafanua kwamba kigezo fulani kinaweza kuakisi mafundisho ya Biblia juu ya asili ya Kanisa na wakati mwingine kinaweza kisiakisi moja kwa moja mafundisho hayo ya Biblia. Ingawa vyanzo hivi na vingine visivyo vya kibiblia (yaani, vyanzo vingine nje Maandiko yenyewe) ni muhimu, haviwezi wala havipaswi kuchukuliwa au kuonekana kuwa muhimu kama ushuhuda wa Biblia yenyewe juu ya asili ya Kanisa. Kwa hiyo, hakikisha kwamba unaweka mazungumzo yote kuhusu vigezo vya kweli vya Kanisa katika msingi wa Maandiko. Njia tunayotumia kugundua kazi ya Kanisa (yaani, kutazama mifano au taswira za Kanisa katika Agano Jipya na kupata mahitimisho kutokana na taswira hizo), inastahili maelezo fulani. Hata mtazamo wa harakaharaka katika taswira mbalimbali za Kanisa katika Agano Jipya unaonyesha kwamba kuna taswira na dhana nyingi, na hizi zote zinawakilisha ufahamu tofauti tofauti na unaohusiana kuhusu Kanisa ni nini na linafanya nini. Katika kitabau cha ajabu na muhimu juu ya Kanisa, Images of the Church in the New Testament, [yaani Picha za Kanisa katika Agano Jipya], Paul Minear anabainisha picha 96 tofauti za Kanisa katika Agano Jipya. Kati ya picha hizi, Minear anaweka picha kadhaa katika makundi matano anayoita picha ndogo: watu wa Mungu, kiumbe kipya, ushirika katika imani, na mwili wa Kristo. Utajiri wa picha hizi unaonyesha kwamba kuna utajiri mkubwa wa maarifa ambao unasubiri kuchimbwa katika picha hizi. Kujifunza Kanisa
9 Ukurasa 131 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
10 Ukurasa 132 Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook - Share PDF online