Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 6 3

THEOLOJIA YA KANISA

kupitia utofauti huu mkubwa wa picha ni kazi ya kila mwanafunzi makini wa Biblia. Kutakuwa na picha nyingi ambazo kwa bahati mbaya hazitapewa uangalifu wowote unaostahili sana: watu wa milki ya Mungu, chumvi ya dunia, taifa takatifu, waraka wa Kristo, matawi ya mzabibu, mke mteule, bibi arusi wa Mwana-Kondoo, wageni na wapitaji, ukuhani wa Mungu, uumbaji mpya, watumwa waliotakaswa, marafiki, na nguzo na msingi wa kweli. Inatosha kusema kwamba Mungu alitupa picha hizi zenye utajiri ili tujishughulishe na kujifunza kwa kina na kwa namna endelevu, tupate kuwaelewa watu wake kupitia picha hizo. Kundi hili tajiri la picha hufanya iwe muhimu na lazima kutambua asili ya Kanisa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia picha halisi tunayojifunza. Tunawahimiza wanafunzi wote wa Maandiko kufuata njia hii, sio tu kwa lengo la kulielewa Kanisa, bali pia kuelewa mafundisho yote makuu ya Maandiko. Waamini wanapigana na Ibilisi, malaika wa kwanza wa viumbe wa Mungu ambao kwa kiburi na kutamani utukufu wa Mungu, walimwasi Bwana Mwenyezi na kuwa adui wa Mungu na wa wanadamu. Wengi huhusisha nafsi ya Shetani na maandiko ya Isaya 14:12-14 na Ezekieli 28:12-15, ambayo yanamwelezea malaika huyu mkuu kuwa “Lusifa” na “Kerubi aliyetiwa Mafuta” kabla ya kuasi na kuanguka kwake. Katika Ufunuo wa Yohana, Shetani anaonekana kuwa aliongoza idadi kubwa ya roho nyingine nyuma yake katika uasi dhidi ya Mungu (Ufu. 12:4), mojawapo ya visa vingi vinavyo mwonyesha akiishi sawa na jina la “Yule Mwovu” na “Mjaribu.” Kulingana na Maandiko, Ibilisi kupitia udanganyifu wake wa uongo alisababisha anguko la wanadamu kama “Nyoka” (Mwa. 3). Katika kile ambacho wanatheolojia wanakiita protoevangelium , tunaona tamko kuhusu uharibifu wa mwisho wa shetani kupitia uzao uliotiwa mafuta wa Mungu (Mwa. 3:15), tendo ambalo lilitimizwa kupitia kazi ya Yesu Kristo msalabani, kama Christus Victor (yaani, Kristo Mshindi) ambapo alimshinda shetani na wafuasi wake, na kuzindua “mwanzo wa mwisho” wa utawala wa Ibilisi, na kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu (Yoh. 12:13-33; rej. Kol. 2:15). Waamini wamekombolewa kutoka katika ufalme wa giza na kuingia katika Ufalme wa nuru kupitia Yesu Kristo (Kol. 1:13), na “wameingizwa” katika jeshi la Mungu kama askari katika vita vya ulimwengu vya Mungu ili kuurudisha ulimwengu mikononi mwake, kwa ajili yake na watu wake. Ijapokuwa shetani amehukumiwa na kushindwa kabisa kwa damu ya msalaba (Kol. 2:15), bado anaendelea kufanya

 11 Ukurasa 137 Kipengele namba III

Made with FlippingBook - Share PDF online