Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 6 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

kazi katika enzi hii na katika ulimwengu huu akiwadanganya wale wasioamini (2 Kor. 4:4), akiwashtaki watakatifu mbele za Bwana (Ufu. 12:10), na kuwajaribu wanadamu kupitia udhibiti alionao juu ya ulimwengu (1 Yoh. 2:15-17; 5:19). Waamini wanapaswa kuwa macho na kuwa na kiasi kwa sababu shetani anatafuta wale ambao hawana ufahamu ili kuwaangamiza, na kudhoofisha kazi ya Mungu kila upande (1 Pet. 5:8). Kazi hii ya majaribu, mashtaka, udanganyifu, na uharibifu ni ya ulimwenguni kote na ya kimfumo, inaratibiwa katika mfumo wa ulimwengu na kupitia mtandao wake wa mashetani wanaofanya kazi chini ya mamlaka yake pamoja na wale wasioamini (Isa. 14:12-17; 2 Kor. 4:3-4; Efe. 2:2; Kol. 1:13). Sehemu muhimu ya kazi ya Kanisa ni kupigana na adui, Ibilisi, kupitia kulitangaza Neno la Mungu. Tuko katika vita endelevu na shetani na wasaidizi wake (Efe. 6:11-18) wanaotafuta kutufanya tusiwe na matokeo kwa njia ya mashambulizi ya moja kwa moja, uongo, udanganyifu, na ukandamizaji, kimwili na kiroho (1 Kor. 5:5; 1 Yoh. 5:16). Tunashinda ghadhabu yote ya kishetani na ya kipepo kupitia damu ya Mwana-Kondoo na neno la ushuhuda wetu (Ufu. 12:11), tunapochukua silaha za Mungu na kusimama dhidi ya hila zake wakati wa uovu (Efe. 6:11-18). Kufundisha kuhusu taswira hizi muhimu za Kanisa kutahitaji matumizi bora ya wakati. Kila taswira ina vipengele vinavyohitaji uchunguzi wa kina na mapana. Kwa sababu hiyo, kwa faida ya usimamizi wa muda, itakuwa muhimu kuamua ni muda gani utatoa kwa kila taswira. Inaweza kuthibitishwa kwa urahisi kuwa Roho Mtakatifu hutupatia taswira mbalimbali ili tuweze kupata upeo wa maarifa kutoka kwa kila taswira. Mitume hawakuona uhitaji wa kuzungumzia kila picha au taswira kwa kila kutaniko au kikundi cha makusanyiko katika kila waraka. Badala yake, walizitumia picha hizo ili kutoa mahusia na mafundisho kwa makanisa kuhusu nyanja mbalimbali za maisha binafsi na mahususi ya kusanyiko husika, na kile walichohitaji kubadilisha au kufanya ili kutatua tatizo fulani, au kutatua mvutano fulani wa kimahusiano. Tumia nyakati za majadiliano kuwaonyesha wanafunzi wako jinsi ya kuchambua na kutafakari picha hizi ili kutimiza wajibu wa kichungaji na ushauri. Hivi ndivyo mitume walivyofikiri, na unaweza kutumia ufundishaji wako kuhusu picha hizi kufikiri kama walivyofikiri – au angalau, kuiga mbinu zao.

 12 Ukurasa 142 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Share PDF online