Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 6 5

THEOLOJIA YA KANISA

Katika kujadili maswali ya kipengele hiki cha kutendea kazi somo na matokeo yake kwa wanafunzi, itakuwa muhimu kuwasaidia wanafunzi kuielewa hekima ya Roho Mtakatifu katika kutupatia taswira mbalimbali. Mitume hawakujaribu kuzioanisha au kuziainisha (yaani kuweka taswira hizi katika makundi); walizitumia kwa uhuru kushughulikia masuala au mahitaji mahususi, au tu kwa lengo kutupatia ufahamu mzuri zaidi wa asili ya kusanyiko la Mungu. Unapojibu maswali pamoja na wanafunzi, wasaidie kuelewa jinsi alama na taswira hizi zinaweza kuwa rasilimali yenye thamani ya kutusaidia kuelewa asili ya Kanisa. Zingatia kwa umakini maswali ya wanafunzi, huku ukitumia nafasi hizo kama fursa kuwasaidia waelewe jinsi mitume walivyotumia “picha” na “taswira.” Kilicho muhimu katika kulitumia Neno la Mungu kwa hali maalum ni uwezo wetu wa kuwa wazi katika namna tunavyoshughulika na Maandiko, wakati huo huo, tukiyaheshimu vya kutosha ili kuyafafanua kwa uangalifu na heshima. Katika kuzingatia uzoefu na hali mbalimbali za mifano hii halisi, ni vyema kufikiria jinsi unavyoweza kuwawezesha wanafunzi kufikiria taswira na picha za Kanisa katika Kazi kama maktaba ya picha kwa ajili ya rejea ili kukabiliana na matatizo na changamoto mahususi. Kila picha na taswira ina hazina yenye utajiri wa maana, tafsiri, na miunganiko, ambayo yote inaweza kutusaidia kuelewa sisi ni nani na tunapaswa kuwaje katika hali fulani. Kuwa kusanyiko la Kikristo ni kuishi kwa kudhihirisha utambulisho ambao Roho Mtakatifu ametupatia kupitia picha nyingi za Kanisa katika Agano Jipya. Unapozingatia mifano hii kwa umakini, fikiria jinsi taswira na picha zinaweza kukuwezesha wewe na wanafunzi wako kufikiria kwa ubunifu na kwa uwazi kuhusu jinsi ya kutambua na kushughulikia matatizo au masuala katika upandaji kanisa na ukuaji wa kanisa kupitia uelewa mpya wa picha za Biblia za Kanisa. Kama ilivyo kwa somo lolote katika mtaala wa Capstone, somo hili linasisitiza ujuzi muhimu ambao viongozi wote wanapaswa kuwa nao ili kufanya kazi kwa ufanisi katika Kanisa. Picha na taswira ambazo Mungu ametupatia za utambulisho wa kweli na kazi halisi ya Kanisa sio tu kwa ajili ya majadiliano na kutafakari. Kinyume chake, taswira hizi zinaunda kolagi, mchoro wa maana unaofafanua asili hasa ya Kanisa. Viongozi wa Kikristo wanapaswa kuelewa na kutumia maana hizi katika

 13 Ukurasa 144 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

 14 Ukurasa 145 Mifano Halisi

 15 Ukurasa 147 Kuhusianisha Somo na Huduma

Made with FlippingBook - Share PDF online