Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 6 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
kila ngazi ya huduma za kusanyiko lao la mahali pamoja, ikijumuisha mahubiri yao, mafundisho, ushauri, usimamizi na uongozi. Unapowawezesha wanafunzi wako kufanya uhusianishaji kati ya maarifa ya moduli hii na huduma za wanafunzi wako, wasisitizie tena hitaji la wao kuwa wataalam katika ujuzi wao wa taswira za Kanisa, na pia katika uwezo wao wa kutumia maana ya picha hizo kwa kila awamu na hatua ya maendeleo na maisha ya Kanisa. Unapojadiliana nao kuhusu namna watakavyotumia maarifa haya, sisitiza tena jukumu hili muhimu la uongozi wa Kikristo, na wape changamoto tena wapate kugundua njia wanazoweza kupata ufahamu wa kina wa dhana hizi na kuzitumia kivitendo mara nyingi wawezavyo. Hongera! Sasa umefika mwisho wa moduli ya Kanisa. Kazi yako kama mkufunzi na mtayarishaji wa maksi na viwango vya ufaulu inaanza sasa. Hakikisha kwamba umepokea kutoka kwao mapendekezo yao kuhusu Kazi ya Huduma kwa Vitendo na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko, pamoja na taarifa nyingine yoyote ambayo itakuwa muhimu kwako katika kuamua daraja la jumla la mwanafunzi. Mara nyingine tena, busara yako kuhusu kazi zilizochelewa inaweza kuamua kwa urahisi ikiwa utawapunguzia wanafunzi alama, jambo ambalo litasababisha mabadiliko ya daraja baadaye, au kuwapa wanafunzi alama ya “haijakamilika” hadi kazi ikamilike. Vyovyote utakavyotekeleza kanuni zako kuhusiana na kazi zao, kumbuka kwamba kozi zetu kimsingi hazihusu maksi ambazo wanafunzi wanapata, bali ile lishe ya kiroho na mafunzo ambayo kozi hizi zinatoa. Pia, hata hivyo, kumbuka kwamba kuwasaidia wanafunzi wetu kujitahidi kupata matokeo bora ni sehemu muhimu ya masomo yetu. Kwa kila jambo, hakikisha kwamba wanafunzi wako wanajiandaa vyema kwa kazi iliyosalia na kwamba wasiwe wazembe au wavivu katika hatua hii ya kozi. Siku zote ni ngumu kumaliza kwa nguvu, lakini hiyo ndiyo changamoto kwao. Watavuna mavuno ya baraka, ikiwa hawatachoka na kukata tamaa (Gal. 6:9). Wahimize kukamilisha kazi zao kwa nguvu na ustadi, na uwe kielelezo kwao katika namna yako ya kufundisha masomo haya na namna unavyoshughulikia mitihani yao.
16 Ukurasa 148 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online