Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

4 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

makanisa yetu, kwenda nje ya mipaka inayokubalika ya namna ibada inavyoeleweka na waamini wa kanisa lako inaweza kumaanisha nini? Je, kuwe na mipaka katika namna tunavyofanya ibada, na ikiwa ndivyo, ni vipi vinapaswa kuwa viwango vya kusimamia mipaka hiyo kwa kuzingatia uhuru wetu katika Kristo, na shauku yetu ya kuonyesha upendo wetu kwa Mungu kwa njia mpya na za kipekee? Liturujia Inachosha Sana – Je, Mungu Anafurahishwa Tukiwa na Huzuni? Wakati wa chakula cha jioni, mmoja wa watoto wa familia fulani ya kanisani alitoa maoni yake kuhusu ibada ya kanisa. Kwa maoni yake ya umri wa miaka 13, ibada za kanisa zilikuwa rasmi sana, zenye kufanana sana, na zenye lugha na shughuli nyingi ambazo hazikuwa na maana yoyote kwake. Alishangaa ni kwa nini hasa nyimbo zilikuwa za zamani sana, na muziki ulikuwa kama wa kwendea mochwari. Mazingira yote yalionekana kuwa ya kusikitisha na kuhuzunisha; hakujua kwa nini walipaswa kurudia maneno, na kuimba nyakati fulani, kusimama wakati fulani, na kusoma nyakati nyingine. Yote haya yanachosha na ni ya kizamani sana. Aliwauliza ndugu zake kwa nini kanisa haliwezi kuwa lenye kusisimua zaidi, kama vile maonyesho ya michezo kwenye TV, au msisimko kwenye matukio ya riadha. “Je, Mungu anapenda tuwe na huzuni?” Aliuliza. Je, unaweza kumwambia nini mtoto huyu wa miaka 13 kuhusu uzoefu wake wa ibada katika kanisa lake, na jinsi Mungu anavyomtaka aelewe na kuitazama ibada ya pamoja?

3

2

Kanisa katika Ibada Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Terry G. Cornett

Neema ya Mungu huja kabla ya uamuzi au juhudi zozote za mwanadamu – ni neema yake pekee ndiyo inayoweza kuwawezesha watu kumwitikia. Ni kwa sababu ya neema hii Kanisa linaweza kumwabudu Mungu, na ibada zote za Kanisa, hasa Meza ya Bwana na ubatizo, zinakusudiwa kuwa ushuhuda na uzoefu wa neema ya Mungu Lengo letu katika sehemu hii ya kwanza ya somo hili la Kanisa katika Ibada ni kukuwezesha: • Kutoa tafsiri ya neema.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Share PDF online