Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 5 1
THEOLOJIA YA KANISA
a. Efe. 2:8-9
b. Mdo. 20:24
c. Gal. 2:21
d. Tendo lolote jema au la haki tunalotenda ni matokeo ya neema ya Mungu inayofanya kazi ndani yetu. Matendo mema ni matokeo ya wokovu sio sababu yake. Hakuna tendo lolote jema linalotupatia kibali chochote cha ziada mbele za Mungu. Hakuna yeyote anayeweza kuwa mwema kiasi cha kutosha ili kupata uhusiano na Mungu au uzima wa milele pamoja naye katika Ufalme wake. Tumemiminiwa neema yake kwa sababu ya Kristo na yale ambayo kazi yake imetutendea. Matendo yetu mema ni mwitikio kwa neema ambayo Mungu ametupa. Tena, Kama vile Mtume Yohana anavyosema, “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza” 1 Yoh. 4:19. Mara zote ibada ni jukumu pekee na la muhimu zaidi la Kanisa kwa sababu ni mahali pa kuanzia kuishi kwa neema. Katika ibada, tunatambua kama vile Yakobo alivyoandika katika Waraka wake kwamba, “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga” Yak. 1:17a. A. Matukio mawili muhimu katika ibada ya Kikristo (mlo na kuoga) Katika kila utamaduni wa Kikristo, Meza ya Bwana na ubatizo ni sehemu muhimu za namna tunavyopata uzoefu wa neema ya Mungu itendayo kazi miongoni mwetu. Hata hivyo, Wakristo wanatofautiana kuhusu namna matendo haya ya ibada yanavyoidhihirisha neema ya Mungu katika Kanisa. Baadhi ya makanisa huita Meza ya Bwana na ubatizo kama “sakramenti” na wanayaelewa mambo hayo kama “njia ya neema” wakati wengine huyaita “maagizo” na kuyaelewa kama ushuhuda wa neema ya Mungu. Wacha nieleze tofauti.
2
II. Ibada ni Mwitikio wa Kanisa kwa Neema ya Mungu.
ukurasa 233 9
Made with FlippingBook - Share PDF online