Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

5 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

3. Katika Maandiko ya Agano Jipya, neema ina maana ya kwamba Mungu anashughulika na sisi kama vile tu anavyoshughulika na Mwanawe Yesu. Kwa hiyo, hakika neema ni kibali cha bure na kisichostahiliwa.

D. Je, tunamaanisha nini tunaposisitiza kuwa kila kitu tulicho nacho ni Sola Gratia , kwa neema pekee?

1. Kwanza kabisa, tunamaanisha kwamba kila mwanadamu ambaye amewahi kuishi anakuja ulimwenguni akiwa amefungwa chini ya dhambi na yuko katika hali isiyo na matumaini kabisa, Rum. 3:10-12. Fundisho potofu au uzushi wa Pelagiani ni imani kwamba mtu hajazaliwa na asili ya dhambi na anaweza kumtafuta na kumwamini Mungu kabisa kwa hiari yake mwenyewe. Kanisa limekataa fundisho la Wapelagiani na badala yake kufundisha kutoka katika Maandiko kwamba mtu anaweza kumjia Mungu kwa sababu tu neema ya Mungu inatenda kazi ndani yake. Ikiwa mtu yeyote anasema kwamba neema ya Mungu inaweza kutolewa kama matokeo ya maombi ya mwanadamu, na kwamba sio neema yenyewe ndiyo inayotufanya tumwombe Mungu, basi atakuwa anapingana na nabii Isaya, au Mtume Yohana ambaye anasema jambo lile lile, “Nilikuwa tayari kujionesha kwao wasiouliza habari zangu. Nilikuwa tayari kuwapokea wale wasionitafuta” . . . Dhambi ya mwanadamu wa kwanza imenyong’onyesha na kudhoofisha sana hiari yake kiasi ambacho baada ya hapo hakuna mtu anayeweza kumpenda Mungu kama inavyompasa au kumwamini Mungu au kufanya mema kwa ajili ya Mungu, isipokuwa neema ya rehema ya Mwenyezi Mungu imemtangulia. ~ Baraza la Orange (529 B.K)

ukurasa 232  7

2

2. Pili, tunamaanisha kwamba kwa kuwa wokovu huja kwa njia ya imani pekee, hauwezi kupatikana na mtu yeyote kwa jitihada binafsi. Wokovu unaweza kupokelewa kama zawadi ya bure tu, ambayo mtu hawezi kuistahili kupitia matendo ya wema. Wokovu ni zawadi kamili ya neema ya Mungu.

ukurasa 233  8

Made with FlippingBook - Share PDF online