Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 5 3

THEOLOJIA YA KANISA

ambayo Mungu alitupa kupitia maisha, kifo na ufufuo wa Yesu na inatukumbusha kwamba Kanisa lipo na linaishi kupitia neema hii.

III. Ubatizo: Ubatizo Unahusianaje na Wokovu?

A. Wale wanaotazama ubatizo kama sakramenti wanauona kama njia ambayo kwayo neema ya Mungu inaleta wokovu. Katika theolojia ya sakramenti, ubatizo ni muhimu kwa ajili ya kuzaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili.

1. Msaada wa Maandiko kwa mtazamo wa ubatizo kama sakramenti au njia ya neema:

2

a. Mdo. 2:38

b. Mdo 22:16

c. Mk. 16:15-16

d. 1 Pet. 3:20-22

“Kanuni thelathini na Tisa za Dini” ambazo ni ukiri wa msingi wa makanisa yenye mapokeo ya KiMethodisti na ya KiAnglikana inaelezea fundisho la kisakramenti la Ubatizo kama hivi: “Wale wanaopokea Ubatizo katika namna sahihi wanapandikizwa katika Kanisa; ahadi za ondoleo la dhambi, na kufanywa wana wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu zinatiwa sahihi na kutiwa muhuri; Imani inathibitishwa, na Neema inaongezeka kwa nguvu ya maombi kwa Mungu.”

~John H. Leith, wah. Creeds of the Churches. Louisville: John Knox Press, 1983. Uk. 275-76

Made with FlippingBook - Share PDF online