Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
5 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
2. Ni muhimu kuelewa kwamba wale wanaotazama ubatizo kama sakramenti hawafundishi habari ya kuzaliwa upya au mara ya pili kwa njia ya ubatizo. Kuzaliwa upya kwa njia ya ubatizo ni imani potofu inayodai kwamba ni ubatizo pekee unaomwokoa mtu kwa sababu tu tendo la ubatizo limefanywa. Nyakati fulani huko nyuma, Kanisa Katoliki lilionekana kufundisha jambo lililokuwa likikaribiana sana na hili, lakini leo mafundisho ya Kikatoliki na Kiprotestanti yanakubali kwamba jambo kuu katika ubatizo ni imani. Baba wa Kanisa Gregori wa Nyssa alisisitiza kwamba ikiwa mtu anabatizwa lakini hakuuambatanisha ubatizo na toba ya kweli basi, “katika hali ya namna hii maji hubaki kuwa maji tu, kwa maana kipawa cha Roho Mtakatifu hakionekani kwa njia yoyote ndani yake yeye ambaye amezaliwa namna hiyo kupitia ubatizo.”
ukurasa 234 13
2
B. Wale wanaofafanua ubatizo kama agizo wanautazama kama ishara ambayo mtu hutangaza utambulisho wake katika Kristo na Kanisa lake. Ubatizo ni muhimu kwa mtu kuingizwa katika Kanisa.
1. Msaada wa Maandiko kwa mtazamo wa ubatizo kama agizo au ishara:
a. Mdo. 10:47
b. 1 Kor. 1:14-17
2. Kichocheo kikuu cha ubatizo ni utii. Kamusi ya Biblia ya Holman, ambayo inawakilisha mapokeo ya Wabaptisti , inasema: Ubatizo si kigezo kwa ajili ya kupata wokovu, bali ni takwa la utii. Ubatizo ni hatua ya kwanza ya ufuasi. Ingawa maana zote za ubatizo ni muhimu, maana moja ambayo mara nyingi huja akilini ni ubatizo wa maji kama picha ya kumjua Kristo kama Bwana na Mwokozi. Ubatizo kamwe si tendo lenyewe la wokovu lakini, badala yake, ni ishara ya tendo lenyewe. Kwa hiyo kielelezo
Made with FlippingBook - Share PDF online