Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

6 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

Meza ya Bwana haina nguvu ya kumzaa mtu upya/mara ya pili, haina neema ya utakaso. Hakuna kitu cha kichawi au cha ajabu kuhusu asili yake. Ni ishara ya uhusiano wa mwamini na Kristo, ambaye peke yake hufanya utakaso. Ishara za nje zilizobuniwa na Kristo mwenyewe ni ishara za nguvu ya upatanisho na upendo wa msamaha wa dhabihu yake kuu, ambayo ilileta mtokeo mara moja na kwa zote. ~ Williams Stevens. “The Lord’s Supper.” Readings in Christian Theology. Millard Erickson, mh. Grand Rapids: Baker, 1973.

b. Lk. 22:19

c. 1 Kor. 11:23-24

2

F. Kile kinachofanana katika mitazamo hii inayotofautiana kuhusu Meza ya Bwana:

1. Kila sehemu ya theolojia ya Kikristo inaamini kwamba Meza ya Bwana ni:

a. Sehemu muhimu ya ibada ya Kikristo.

b. Amri ya moja kwa moja ya Kristo kwa Kanisa lake.

c. Wasaa unaotusogeza karibu zaidi na Mungu na waamini wenzetu.

d. Wasaa unaoturuhusu kushika neema ya Mungu na kumwitikia kwa shukrani na sifa.

e. Ilikusudiwa kupokelewa kwa imani na kutusaidia kuweka imani zetu kamili katika kazi ya Kristo.

Made with FlippingBook - Share PDF online