Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 6 1

THEOLOJIA YA KANISA

f. Wasaa ambao dhambi zinaweza kushughulikiwa na kuwekwa chini ya rehema ya Mungu yenye kusamehe.

2. Tunaweza kutokubaliana juu ya namna Meza ya Bwana inavyosababisha mambo haya kutokea lakini kutoelewana huko kusitufanye tusahau umuhimu wa msingi wa Mlo huu katika maisha yetu ya ibada. Ni zawadi ya neema ya Mungu kwa Kanisa lake.

Hitimisho

» Kuabudu ni mwitikio wa Kanisa kwa neema ya Mungu.

» Wokovu hupatikana kwa neema ya Mungu na hakuna mwanadamu anayeweza kusema kwamba amejipatia wokovu wake kwa yale aliyoyafanya.

2

» Ubatizo na Meza ya Bwana ni sehemu muhimu sana za ibada ya Kikristo.

» Kanisa linatofautiana kwenye namna ya kuielewa Meza ya Bwana na ubatizo. Wengine wanaamini kwamba ni sakramenti, yaani, njia ambayo neema ya Mungu inatujia huku wengine wakiamini kwamba ni maagizo ambayo yanaashiria na kushuhudia neema ya Mungu.

Tafadhali chukua muda mwingi kadiri uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameletwa na video. Maswali haya yaliundwa ili kukusaidia kupitia maudhui ya somo hili kuhusiana na neema ya Mungu kama msingi wa ibada ya Kanisa. Unapojibu maswali haya, jaribu kuunda uthibitisho wa wazi juu ya kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu neema ya Mungu. Kwa kuwa Wakristo wanaoamini Biblia hutofautiana kuhusu namna neema ya Mungu inavyotujia katika Meza ya Bwana na ubatizo, tafadhali wasikilize kwa karibu na kwa heshima wale ambao wanaweza kutokubaliana nawe darasani. Jibu kwa uwazi na kifupi, na inapobidi tetea jibu lako kwa Maandiko! 1. Sola Gratia inamaanisha nini na kwa nini ni muhimu? 2. Uzushi wa Pelagiani ni nini?

Sehemu ya 1

Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

ukurasa 236  19

Made with FlippingBook - Share PDF online