Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
6 2 /
THEOLOJIA YA KANISA
3. Kuna tofauti gani kati ya mapokeo ya Kikristo yanayoelezea ubatizo na Meza ya Bwana kama sakramenti na yale yanayozichukulia kama maagizo ? 4. Je, kuna hoja zipi kuu za kibiblia zinazokubaliana na zinazotofautiana na suala la kuona ubatizo kama «njia ya neema»? 5. Je, kuna maoni gani makuu manne kuhusu Meza ya Bwana? 6. Kwa nini imani kwamba kubatizwa husababisha wokovu ni fundisho lisilo la kimaandiko? Je, hili linatofautianaje na mtazamo wa kisakramenti wa ubatizo? 7. Kwa nini wanamatengenezo Waprotestanti hawakukubaliana na fundisho la Kikatoliki la ex opere operato ? 8. Je, imani ina nafasi gani katika uzoefu wetu wa sakramenti/maagizo?
2
Kanisa katika Ibada Sehemu ya 2: Wito wa Kanisa
Mch. Dkt. Don L. Davis
Wito halisi wa Kanisa ni kumwabudu Mwenyezi Mungu. Tunamtukuza Mungu katika ibada yetu kwa sababu ya tabia yake kamilifu – utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani na kazi zake zisizoweza kulinganishwa na chochote. Kanisa linamwabudu Mungu wa kweli, Mungu wa Utatu kupitia Yesu Kristo. Tunamwabudu Yehova Mungu pekee, kupitia Yesu Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa kuongezea, Kanisa humwabudu Mungu kwa njia ya sifa na shukrani, kwa njia ya liturujia, ambayo inasisitiza Neno na sakramenti, na kwa utiifu wetu na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano. Lengo letu la sehemu hii, Wito wa Kanisa , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Tunaabudu ili kumtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani na kazi zake zisizoweza kulinganishwa na chochote.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook - Share PDF online