Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 6 3
THEOLOJIA YA KANISA
• Tunamwabudu Mungu wa Utatu kwa njia ya Yesu Kristo. Tunamwabudu Yehova Mungu pekee, kupitia Yesu Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. • Tunaabudu kwa njia ya sifa na shukrani, kupitia liturujia, ambayo inasisitiza Neno na sakramenti, na kupitia utiifu wetu na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano. I. Sababu kuu kwa nini kusudi la Ibada ya Kanisa ni kumtukuza Mungu Mmoja, wa Kweli, na Mwenyezi, Yahweh. Kama Israeli wa zamani, Kanisa lipo kwa ajili ya utukufu na raha ya juu ya Mungu, na vyovyote Kanisa lilivyo na katika lolote lifanyalo linapaswa kulifanya ili kumtukuza Mungu katika mambo yote. Paulo anaeleza jambo hili mara nyingi katika Agano Jipya, akisisitiza, kwa mfano: “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye” (Kol. 3:17). “Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.” Na tena katika mstari wa 21, “watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu” (Isa. 43:7, 21). “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.” (1 Pet. 2:9-10). Hasa hasa, kwa nini basi tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mkuu na mtukufu? Majibu yanatokana na utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani, na matendo yake yasiyo na kifani.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
ukurasa 237 20
2
A. Tunamwabudu Mungu kwa sababu yuko peke yake katika utakatifu .
1. Isa. 6:3
Made with FlippingBook - Share PDF online