Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 7 1
THEOLOJIA YA KANISA
1. Kulingana na sehemu hii, ni sababu gani kuu na muhimu ambayo inalifanya Kanisa la Yesu Kristo lijihusishe na ibada kama shughuli yake muhimu zaidi na wito wake halisi? 2. Ukweli kwamba Mungu aliumba vitu vyote kwa ajili ya heshima, utukufu, na raha yake unaathirije msukumo wa Kanisa katika kumwabudu Mungu? 3. Toa ufafanuzi kuhusu ukweli kwamba Kanisa linamwabudu Mungu kwa sababu ya ukuu wa tabia yake na matendo yake. Ni sifa gani hasa za Mungu zinazodai na kutuita tumwabudu? 4. Kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba Kanisa humkaribia Mungu katika ibada kupitia Yesu Kristo na kazi yake pekee? Je, inaweza kuwa vinginevyo? Elezea jibu lako. 5. Je, Roho Mtakatifu anaongezaje na kutia nguvu ibada ya Kanisa linapotafuta kumtukuza Mungu kwa njia ya sifa zake? Kanisa linapataje nguvu za Roho linapompa Mungu utukufu? 6. Ni njia zipi ambazo Kanisa linaweza kumwabudu Mungu: Katika utiifu wake na mtindo wake wa maisha? Katika liturujia yake, hasa katika kuhubiri Neno na kushika maagizo (sakramenti)? Katika miundo na misemo yake, kimwili na kimuziki? 7. Matendo ya upendo, kujaliana na kutunzana ndani ya kanisa yanaathirije ibada ya Mungu kupitia kanisa? Je, kanisa linaweza kumwabudu Mungu ikiwa uhusiano kati ya washirika wake ni wa mvutano na umevurugika? Eleza. Somo hili linaangazia njia ya msingi ambayo sisi kama washirika wa Kanisa tunayo katika kumkaribia Mungu, yaani, ule msingi wa neema pekee kwa njia ya imani katika Kristo, na jinsi uzoefu wa neema hii unavyojidhihirisha katika sifa, kuabudu, shukrani na ibada ya kweli kwa Mungu kupitia Yesu Kristo. Katika maana moja, kuelewa dhana hizi za msingi ni kiini cha maana halisi ya kulitumikia Kanisa kama mmoja wa viongozi wake, na hutusaidia kung’amua wakati kusanyiko lina afya au linaumwa, kulingana na uzoefu wake wa kibali na neema ya bure ya Mungu katika Kristo, na udhihirisho hai wa shukrani yake kupitia njia yake ya maisha katika ibada. Zifuatazo ni baadhi ya dhana za msingi zinazohusiana na ibada, wito wa kweli wa Kanisa.
2
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
ukurasa 241 24
Made with FlippingBook - Share PDF online