Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

7 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

³ Wokovu ni zawadi ya bure kabisa ya Mungu inayopaswa kupokelewa kwa imani na haiwezi kupatikana kwa jitihada au kwa kustahili. ³ Wanadamu wamefanywa watumwa wa dhambi kiasi kwamba hawawezi kutamani mambo yaliyo sahihi isipokuwa neema ya Mungu ifanye kazi ndani yao kwanza. ³ Mara zote Mungu ndiye wa kwanza katika kuchukua hatua ya kumleta mtu katika wokovu. “Sisi tunampenda kwa sababu yeye alitupenda sisi kwanza.” ³ Kwa sababu Kanisa ni jumuiya ya watu ambao wanauzoefu wa neema ya Mungu, ibada ni wajibu na furaha ya Kanisa. ³ “Mlo na kuoga” (Meza ya Bwana na ubatizo) ni sehemu ya namna ambayo tunashiriki na kukumbuka neema ya Mungu. Hivi ni vipengele muhimu vya ibada ya Kikristo. ³ Sakramenti ni njia ambayo kwayo neema ya Mungu inatolewa kwetu wakati agizo ni tendo linalokubali neema kupitia utii na ukumbusho. Aina zote mbili za theolojia zinasisitiza kwamba kushiriki katika Meza ya Bwana na ubatizo kuna faida ikiwa tu kutaambatanishwa na toba na imani. ³ Viongozi wa Kikristo wanapaswa kusoma Maandiko na kuamua kama ni sahihi kuielewa Meza ya Bwana na ubatizo kama sakramenti au kama maagizo. ³ Wito mkuu wa Kanisa ni kumwabudu Mungu, na sababu kuu kwa nini Kanisa liabudu ni kwa kusudi la kumtukuza Mungu mmoja, wa kweli, na Mweza Yote, Yahweh. ³ Kanisa humwabudu Mungu kwa sababu ya hali isiyo na kifani ya tabia yake kuu na matendo yake makuu kupitia uumbaji na wokovu. Kwa hiyo, Mungu daima anastahili kuabudiwa na kusifiwa na washirika wa Kanisa. ³ Kwa sababu vitu vyote viko kwa mapenzi mema ya Mungu na kwa furaha yake, ibada ya Mungu ndiyo shughuli ambayo viumbe vyote hushiriki katika kusudi lao. Telos (lengo la mwisho) la kila kitu kilichopo ni kumsifu na kumheshimu Mungu kwa jinsi alivyo na kile alichokifanya. ³ Kanisa humwabudu Mungu kwa njia ya ibada zake za sifa na shukrani, na kama makuhani wa kiume na wa kike wa Mungu, humtukuza kwa njia na mbinu mbalimbali, kutia ndani nyimbo, kucheza, kupiga magoti, kunyamaza, kupiga makofi, kupiga kelele, n.k.

2

Made with FlippingBook - Share PDF online