Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 7 3

THEOLOJIA YA KANISA

³ Liturujia ni utaratibu maalum wa Kanisa wa ibada ambapo hutangaza, bila kujali mapokeo, mahubiri na mafundisho ya Neno la Mungu na kusherehekea pamoja katika Meza ya Bwana wakati wote wanapokusanyika. ³ Aina zote za matendo ya Kanisa katika ibada yake zinapaswa kuongozwa na Roho Mtakatifu chini ya mwongozo wa Neno la Mungu. Kila utamaduni ambamo Kanisa limo uko huru na unawajibika kufafanua muziki wake, maadhi, mtindo, na aina ya ibada, kulingana na kanuni na kweli ya Kristo. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu Kanisa katika Ibada. Kuelewa nafasi ya kimkakati ya neema katika kuanzisha uhusiano kati ya Mungu na kusanyiko la waabudu, pamoja na uhuru na wajibu wa kumwinua Mungu ambao Kanisa linao, ni msingi wa kuwa kiongozi wa Mungu leo. Inaweza kusemwa kwamba ni hadi mtu aelewe na aweze kueleza ukweli huu kwa maneno na matendo, ndipo ataweza kutekeleza uongozi bora katika Kanisa. Pitia maswali haya ili kuona kama unaelewa kikamilifu kweli hizi na maana za maudhui haya, na jinsi ukweli huu unavyohusiana na wewe na mahusiano yako katika huduma. Je, una maswali gani hasa katika mwangaza wa maudhui ambayo umejifunza hivi punde kuhusu ufahamu wako mwenyewe wa kweli hizi? Pengine baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Ingawa watu wengi hawajawahi kusikia kuhusu “uzushi wa Pelagiani,” kuna watu wengi wanaoufanya. Ni kwa namna gani mtu ambaye hakuuelewa wokovu kwa njia hii angezungumzia maana ya kuwa Mkristo? * Je, kanisa lako (au dhehebu) linaelewa Meza ya Bwana na ubatizo kuwa ni sakramenti au maagizo? Kwa nini? * Ni mara ngapi kanisa linapaswa kushiriki Meza ya Bwana pamoja? Kwa nini? * Je, ni kwa kiwango gani timu yako ya kuabudu katika kanisa lako inafahamu kikamilifu ukweli na matokeo yanayohusiana na ibada kama wito wa Kanisa? * Pana kiwango gani cha uhuru katika kuabudu katika kanisa lako kwa maana ya matendo ya kimwili na kisaikolojia yanayosisitizwa katika Biblia? Je, maagizo haya ya kupiga kelele, kupiga makofi, na kucheza “vielelezo vya kitamaduni” yapo kwa kiasi gani ukilinganisha na maagizo ya kibiblia ya ibada? Elezea jibu lako.

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

2

ukurasa 241  25

Made with FlippingBook - Share PDF online