Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

7 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

* “Liturujia” ya kanisa lako ikoje, kwa maneno mengine, ni kwa namna gani kanisa lako linapanga ibada na sherehe zake ili “kusimulia Hadithi Kuu” katika ibada zake? Ni nini kinazuia hili kuwa na ufanisi zaidi katika kanisa lako? * Mtu anabadilishaje hali ya kiutamaduni ya kusanyiko kutoka kuwa na ibada isiyoruhusu mabadiliko, iliyozoeleka hadi kuwa na sifa zenye nguvu na zenye uhai? Je, ni hatua gani zinahitajika ili kufikia hali kama hiyo?

MIFANO

Kujionyesha Pasina Sababu

Kanisa la mahali pamoja lenye idadi kubwa ya wanamuziki na waimbaji wenye vipawa, sasa limeanza kukua kupitia huduma ya kuabudu yenye nguvu na ubora wa hali ya juu. Hata hivyo, baadhi ya watu wameanza kulalamika kwa sababu kiongozi wa muziki amefanya iwe ngumu zaidi kwa wale wanaoitwa «waabudu wa kawaida» kuwa kwenye timu ya kuabudu au bendi ya sifa. Waimbaji wote lazima wafanyiwe majaribio kwa ajili ya kupima ubora wa sauti zao na uwezo wao wa kusoma muziki, na hakuna wanamuziki wanaoruhusiwa kujiunga kwenye bendi ya sifa kama hawawezi kusoma muziki na kuufuata mpangilio mzuri (lakini mgumu) wa muziki kwa nyimbo zilizochaguliwa. Kiongozi wa muziki ana msimamo imara kwamba Mungu ni mkuu na kwa sababu hiyo ibada yetu inapaswa kuwa bora zaidi kadiri iwezekanavyo. Je, ungekuwa na ushauri gani kwa kiongozi wa huduma ya muziki endapo angekuomba utoe maoni kuhusu uelekeo wa ibada katika kanisa hili? Kiongozi mpya wa ibada kanisani amekuwa akisisitiza haja ya madhihirisho ya vitendo, ya nje au ya kimwili wakati wa ibada. Ana nguvu sana katika maoni yake kwamba tunapaswa kutumia njia mbalimbali ambazo Maandiko yanazungumza katika kuonyesha upendo wetu kwa Mungu – kupiga makofi, kuinua na kupunga mikono yetu, kupiga kelele, kucheza, kupiga magoti, kunyamaza, kulala kifudifudi, kupiga kelele za furaha – tunapaswa kuonyesha upendo wetu kwa Mungu kwa miili yetu. Kundi dogo lakini lenye msimamo kanisani linapingana vikali na jambo hili, na linataka kukomesha msisitizo huu kuhusu madhihirisho haya ya nje. Kwa sababu kimsingi, huu sio mchezo wa mpira wa miguu, bali ni ibada kwa Mwenyezi Mungu. Mabishano yanazuka miongoni mwa washirika kuhusu kile ambacho kinafaa zaidi kwa kanisa hili. Je, ungewasaidiaje kutatua suala hili? Huwezi Kunifanya Niabudu

1

ukurasa 242  26

2

2

Made with FlippingBook - Share PDF online