Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

7 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo yanayohusiana na mada zilizoletwa katika somo hili la Kanisa katika Ibada , unaweza kujaribu vitabu hivi: Boschman, Lamar. The Rebirth of Music. Shippensburg: Destiny Image, 2000. Bridges, Jerry. Transforming Grace: Living Confidently in God’s Unfailing Love. Colorado Springs, CO: NavPress, 1993. Engle, Paul E. Baker’s Worship Handbook. Grand Rapids: Baker Book House, 1998. Hill, Andrew E. Enter His Courts With Praise! Grand Rapids: Baker Book House, 1993. Oden, Thomas C. The Transforming Power of Grace. Nashville: Abingdon Press, 1993. Webber, Robert. Planning Blended Worship. Nashville: Abingdon, 1998. Sasa ni wakati muhimu katika somo kutafuta kujua ni nyanja zipi za theolojia hii ya kibiblia zinaweza kuwa na matumizi zaidi kwenye maisha yako binafsi. Ni kwenye eneo lipi hasa Roho Mtakatifu anaweza kuwa anakuita ili kuyatumia katika hali yako ya sasa ya huduma mafundisho haya yahusuyo neema ya Mungu, na ibada ambayo ni matokeo ya ufahamu kamili wa neema katika maisha yetu binafsi na kanisa? Kutengeneza uhusiano ulio wazi na wenye nguvu ni ujuzi mkuu wa kiongozi yeyote mwenye sifa, na sasa ni fursa kwako kufanya mazoezi ya ujuzi huu, hasa kwa kuuhusianisha na maisha yako mwenyewe. Tafakari juu ya kweli hizi na uone ni ukweli upi au kweli zipi ambazo unaweza kuhitaji kuzitafakari na kuziombea katika wiki hii yote ijayo. Uwe tayari kwa namna Roho Mtakatifu anavyoweza kukutaka usisitize kweli hizi unapowahudumia wale walio chini ya uangalizi wako wiki hii, na umwombe hekima unapotumia kweli hizi katika mazingira yako. Omba kwa Mungu kwa ajili yako mwenyewe na wale unaowahudumia, ili upate kuelewa hasa na kufahamu nguvu ya neema ya Mungu inayobadilisha maishani mwako na kwenye maisha ya wale unaowafundisha. Mwombe Roho Mtakatifu aufanye upendo wa Kristo kuwa halisi zaidi katika maisha yako binafsi, na utafute uwezo wake kwa namna unavyoweza kuwa huru zaidi katika kuelezea sifa na shukrani zako kwa Mungu kwa jinsi alivyo na kwa yale aliyoyafanya maishani mwako. Zaidi sana mwombe Bwana ufahamu katika mambo hayo, maeneo, tabia,

Nyenzo na Bibliografia

2

Kuhusianisha Somo na Huduma

Ushauri na Maombi

ukurasa 242  27

Made with FlippingBook - Share PDF online