Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 7 7

THEOLOJIA YA KANISA

au mazoea yanayoweza kukuzuia kutoa sifa zaidi na bora kwa Mungu katika maisha yako, kulingana na wito wetu wa kuleta furaha na heshima ya juu kwa Mungu.

MAZOEZI

Waebrania 10:19-22

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kujua kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize Mshauri wako.

Kazi ya Usomaji

2

Tafadhali soma kwa umakini kazi zilizo hapo juu na kama ilivyokuwa kwa wiki iliyopita, ziandikie muhtasari kwa ufupi na ulete muhtasari huo kwenye kipindi wiki ijayo (tafadhali angalia “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Pia, sasa ni wakati wa kuanza kufikiria kuhusu aina ya kazi yako ya huduma, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya Ufafanuzi. Usichelewe kufanya maamuzi kuhusiana na kazi yako ya huduma na ile ya ufafanuzi wa Maandiko. Kadiri utakavyofanya maamuzi mapema, ndivyo utakavyokuwa na muda wa kutosha kujiandaa! Kanisa la Yesu Kristo ni wale wote ambao kupitia imani katika Kristo wameipokea neema ya Mungu na kupata badiliko litokanalo na neema. Neema hii inayobadilisha inawafungua ili kumwabudu na kumsifu Mungu wao mkuu wa upendo, kadhalika inawapa mzigo na shauku ya kuwashirikisha wengine hadithi hii ya ajabu ya Yesu na upendo wake. Katika somo letu linalofuata tutaangazia agizo la Kanisa la kutoa ushuhuda wa Kristo na Ufalme wake kupitia matendo yake na shughuli za utangazaji na uenezi, na jinsi Mungu anavyoliwezesha Kanisa kuwa wakala na mwakilishi wake ulimwenguni kwa njia ya Roho wake.

Kazi Zingine

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook - Share PDF online