Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
8 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
a. Kumb. 10:15
b. Kumb. 14:2
c. Zab. 105:6, 43
d. Isa. 41:8
e. Uteuzi wa Mungu kwa Israeli ili kumwakilisha unaunganishwa moja kwa moja na agizo lake kwao la kuwa watakatifu, kwa kuwa wao kama taifa teule la Mungu lazima waonyeshe tabia yake mwenyewe ya uadilifu.
3
3. Utagundua kwamba Agano la Kale halisemi kwamba watu wa Israeli ni wateule wa Mungu kwa sababu tu ya nasaba na uhusiano wa kiukoo na Ibrahimu.
a. Ndani ya taifa kubwa kuna mabaki watakatifu na wateule wa Mungu mwenyewe.
b. Mungu anawatambua baadhi ya Waisraeli kuwa wateule wake, mabaki ambao wanaunda kundi tofauti ndani ya Israeli kubwa zaidi, Isa. 65:8-9.
c. Isa. 10:20-23 na Isa. 14:1. Bwana Mungu “atamchagua Israeli tena.”
4. Rum. 9-11. Ingawa Injili imekataliwa na Wayahudi wengi, watu waliochaguliwa na Mungu, Mungu atawakomboa mabaki yake, kama ilivyonenwa katika Agano la Kale.
Made with FlippingBook - Share PDF online