Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 8 7

THEOLOJIA YA KANISA

b. Efe. 1:9-10

c. 1 Pet. 1:20

d. Ufu. 1:5-8

3. Yesu alithibitisha jukumu lake kama Masihi mpakwa-mafuta wa Mungu katika ushuhuda wake juu yake mwenyewe kwa wasafiri kwenye barabara ya Emau, na kwa mitume baada ya ufufuo wake, Luka 24:25-27, 44-48.

4. Uchaguzi wa Mungu daima uko katika Kristo, na baraka zote za kiroho tunazopokea tunapokea kwa sababu ya muungano wetu na Kristo na Imani yetu katika yeye.

3

a. Efe. 1:3

b. 2 Pet. 1:3-4

II. Pili, Mungu alijichagulia mwenyewe watu ambao kutoka kwao Masihi angezaliwa, ambao kuptia wao ahadi ya wokovu itatolewa.

A. Taifa la Israeli ni ishara na mtangulizi wa watu wateule wa Mungu.

1. Taifa la Israeli limechaguliwa kuwa milki ya Mungu na kama shahidi wake duniani kote, Kum. 7:6-8.

2. Msisitizo huu huu pia unaonekana katika maandiko mengine muhimu ya Agano la Kale.

Made with FlippingBook - Share PDF online