Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
8 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
2. Mathayo 12:18 fasili ya Isaya 42:1
3. Nyimbo za Mtumishi katika Isaya ni utabiri kuhusu ujio na huduma ya Yesu wa Nazareti.
a. Yesu alihusishwa moja kwa moja na Mtumishi Atesekaye wa kitabu cha Isaya, ambaye kupitia kwake Yehova angewaokoa watu wake, Mt. 8:17 (rej. Isa. 53:7-8).
b. Yesu ndiye Mtumishi wa Yehova anayeteseka, Aliyechaguliwa kuukomboa ulimwengu kwa niaba ya Mungu mtakatifu Yahweh. (1) Mdo 3:13 (2) Mdo 4:25, 27, 30 (3) Mdo 8:32-33
3
C. Yesu pia ni Masihi, Yule aliyechaguliwa na Mungu mwenyewe kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote, aliyeteuliwa kufufuka kutoka kwa wafu, na kuchaguliwa hatimaye kutawala juu ya viumbe vyote.
1. Neno la Paulo linalotumika mara kwa mara “katika Kristo” ni kifupisho katika Agano Jipya kwa ajili ya kuelewa jinsi Mungu anavyoleta uchaguzi wa watu wake.
2. Kulingana na Agano Jipya, Yesu alichaguliwa kutimiza mpango wa Mungu, kwamba Masihi atateswa na kufa, kufufuka tena, na kutawala juu ya uumbaji.
a. Mdo 3:20
Made with FlippingBook - Share PDF online