Theolojia Katika Picha

/ 1 1 9

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuchagua Vigezo vya Uhuru Vinavyoaminika Kuabiri Kuelekea Mpito Wenye Afya Don L. Davis

Ili kuwa na kipindi tulivu cha mpito kutoka kwenye jumuiya inayoongozwa na wamishenari hadi jumuiya ya kanisa la kienyeji linalojitegemea, ni lazima tutambue na kukubaliana juu ya vigezo vya wazi ambavyo vitatusaidia kujua kipindi hicho cha mpito kitakapokamilika. Kwa maneno mengine, kila kitu kinategemea uwezo wa wahusika wakuu wote (yaani, wamishenari, wazee, na jumuiya ya kanisa) kuwa wazi kuhusiana na mawazo yetu kwa habari ya kile ambacho kipindi cha mpito kitahusisha na kile tunachotafuta kutimiza. Ikiwa, kwa sababu yoyote ile, hatuko wazi kuhusu matarajio na mielekeo yetu kwa pamoja, tunaweza kutoelewana kwa urahisi, na kurefusha mchakato, au hata kufanya kipindi cha mpito kuwa kigumu bila sababu. Sifa zifuatazo zimetolewa kama mwongozo, kigezo ambacho kinaweza kutusaidia kama viongozi kutathmini kwa kina ikiwa tumeshughulikia maeneo yote muhimu ya mchakato wa mpito. Orodha hii ni mapendekezo, haina kila kitu, na haikusudiwi kuwa muhtasari wa mambo ya lazima, lakini ni kichocheo cha kutusaidia kufikiria kwa umakini masuala yote muhimu ili kufanya kipindi cha mpito kuwa wezeshi na chenye uwazi. 1. Kundi laWanafunziwaYesuWaaminifu,Walioongoka,Waliokusanyika na Wanaokomaa a. Wokovu thabiti na kuishi kwa ajili ya Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. b. Kujitambulisha kama kusanyiko tofauti la Kikristo lenye hali yake ya kiroho iliyojaa shauku kwa ajili ya Bwana, ibada yenye mvuto, na uwepo thabiti katika jamii. c. Kuwa na uelewa wa kina kuhusu ushirika, na mtazamo wa umiliki, na washirika wanaojitambulisha kama sehemu ya kusanyiko; kuwa na uwezo wa kuleta washirika wapya kwa urahisi kupitia mwenendo thabiti na mahusiano ya upendo. d. Mfumo thabiti wa kuingia katika ushirika, kuwaadibisha washirika, na kuwarejesha. e. Utaratibu mzuri wa kujumuisha watu katika maisha ya Mwili (yaani, maisha ya kikundi kidogo, urafiki, ushirika wa kikundi kikubwa, n.k). 2. Kutambua Viongozi Wenyeji, Kuwasimika na Kuwaingiza Kazini a. Wamechaguliwa na Mwili na kwa ajili ya Mwili, hadharani na kwa maombi. b. Waamuzi wa mwelekeo na uendeshaji wa kanisa. c. Kuwajibika kwa washirika wa kanisa kwa maisha na huduma yao.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software