Theolojia Katika Picha
/ 1 4 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kusonga Mbele Kwa Kuangalia Nyuma Kuelekea urejeshaji wa mapokeo makuu, kiinjili Mch. Dkt. Don L. Davis
Ugunduaji tena wa “mapokeo makuu” Katika kitabu kidogo cha ajabu, ola Tjorhom, 1 kina elezea “mapokeo makuu” ya kanisa (wakati mwingine yanaitwa” mapokeo bora ya kikristo)” kama kiumbe hai na chenye nguvu. 2 Mapokeo makuu huwakilisha kwamba, akiinjili, akimitume na kikatholiko ni kiini cha imani ya kikristo na desturi ambayo ilikuwa imefanikiwa sana kutokea 100-500BK. 3 Utajiri wa urithi wake na hazina huwakilisha ungamo la kanisa yale ambayo kanisa linayaamini kila wakati, ibada ambazo zamani kanisa lisilogawanyika walisherehekea na kuunganisha na utume walioukubali kuufanya. Wakati mapokeo makuu hayawezi kuchukua nafasi ya mapokeo ya kitume (yaani, chanzo cha mamlaka yote ya imani ya kikristo, maandiko), wala hayawezi kufifisha uwepo hai wa kristo katika kanisa kupitia Roho Mtakatifu, bado yana mamlaka na ya natia nguvu kwa watu wa Mungu. Yanao, na bado yanaweza kuwapatia watu wa Mungu kwa nyakati, utajiri wa maungamo yake na imani, mapokeo makuu yamekubalika na kuthibitshwa na wa katholiki, orthodox,, wa Anglicana na watheologia wa kiprotestanti, wale wa zamani na wa kisasa zimekwisha tolewa nyaraka za, mafundisho maungamo na desturi za kanisa. (km; kanuni za maandiko, mafundisho ya utatu na uungu wa Kristo, nk.) Wasomi wengi wa Kiinjili wanaamini kwamba njia ya kusonga mbele kwenye imani yenye nguvu na uamsho wa kiroho italazimu kuangalia nyuma, si kwa kupenda na kuwaza siku nzuri za zamani za bila ustaarabu, za kanisa la kwanza lisilokuwa na matatizo au nyofu na hasa kujaribu kuiga safari yao ya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1 Ola Tjorhom, visible church – visible unity:- Ecumenical Ecclesiology na “The Great Tradition of the Church.” Collegeville, Minnesota:- Liturgical Press, 2004. Robert Webber aliyafafanua mapokeo makuu kwa namba hii:- (ni) ni muhtasari mpana wa imani ya kikristo na desturi iliyoendelezwa kutoka katika maandiko kati ya wakati wa Kristo na katikati ya karne ya tano.”Robet E webber The Majestic Tapstry. Nashville:- Thomas Nelson publishers 1986 p.10
2 Ibid, uk. 35
3 Kiini cha mapokeo makuu yanajikita katika uchanganuaji wa kanuni, maungamo na desturi za karne tano za kwanza za mawaidha na kazi za kanisa. Thomas Oden, katika maudhui yake alidai kuwa “--wingi wa vitu vyenye thamani vya kudumu katika nyakati za mafafanuzi ya kibiblia vilivumbuliwa katika karne ya tano.” (cf. Thomas C. Oden, The Word of Life. San Francisco:- HarperSanFrancisco,1989, p 11)
Made with FlippingBook Digital Publishing Software