Theolojia Katika Picha

/ 1 5 1

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

5. Uwepo katikati wa kanisa. Mapokeo makuu kwa uhakika yanakiri kuwa kanisa ni watu wa Mungu. Kusanyiko la waumini waaminifu chini ya mamlaka ya mchungaji Kristo Yesu, sasa ni nukta na wakala wa ufalme wa Mungu hapa duniani. Katika ibada yake, mafundisho, huduma na ushuhuda Kristo anaendelea kuishi na kutembea. Mapokea makuu yanakazia kwamba kanisa chini ya mamlaka ya Mchungaji na ukamilifu wa ukuhani wa waumini nia makazi yanayoonekana ya Mungu katika Roho katika ulimwengu wa leo. Na Kristo mwenyewe akiwa jiwe la pembeni, kanisa ni hekalu la Mungu mwili wa Kristo na hekalu la roho Mtakatifu. Waumini wote walio hai na waliokufa na wale ambao hawajazaliwa wanaunda Kanisa moja, takatifu Katholiko (la ulimwengu wote), na jamii ya kitume. Wakikutanika pamoja daima katika kusanyiko la waumini, wana kanisa wanakutana mahali pamoja kumwabudu Mungu kwa maneno na sakarmenti, na kushuhudia katika kazi yake njema na kutangaza injili. Wakiwa ingiza waumini wapya kanisani kwa njia ya ubatizo, huthibitisha maisha ya ufalme katika ushirika wake, na kuonyesha katika maneno na matendo uhalisia wa ufalme wa Mungu kupitia maisha yake ya pamoja na huduma kwa auliwengu. 6. Umoja wa imani. Mapokeo makuu yanathibitisha kwa sauti moja ukatholiko wa kanisa la Yesu Kristo, kwa kuwa yanahusika na kushikilia ushirika na mwendelezo wa ibada na thiologia ya kanisa kwa nyakati zote (Kanisa la ulimwengu wote) kwa kuwa kumekuweko na inaweza kuwako tumaini moja tu, wito, na imani, mapokeo makuu yalipigania na kujitahidi kuwa na umoja katika neno katika mafundisho, katika ibada, katika hisani. 7. Mamlaka ya kiinjili ya Yesu aliyefufuka. Mapokeo makuu yanathibitisha mamlaka ya kimitume kulijulisha taifa ushindi wa Mungu katika Kristo ya kutangaza wokovu kwa neema kwa njia ya imani katika jina lake, na kuwaita watu wote kwenye toba na imani kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa matendo ya uadilifu na haki, Kanisa linaonyesha maisha ya ufalme duniani leo, na kwa mahubiri yake na maisha ya pamoja linatoa ushuhuda na ishara ya ufalme uliopo ndani na kwa ulimwengu (Sacramentumundi), Na kwa kuwa ni nguzo na msingi wa kweli. Kama ushahidi wa ufalme wa Mungu na kama walinzi wa neno la Mungu, kanisa limeagizwa kufafanua waziwazi na kutetea imani mwanzo na mwisho kwa kanisa la mitume. Hitimisho:- Kutafuta siku zetu za baadaye kwa kwa kuangalia nyuma. Katika wakati ambapo wengi wamechanganyikiwa kwa kelele za machafuko ya watu wengi wanadai kuzungumza kwa ajili ya Mungu, ni wakati kwetu sasa kugundua tena mizizi ya imani yetu kurudi nyuma mwanzoni kwenye maungamo ya kikristo na desturi, na kuona kama kwa kweli tunaweza kupata tena utambulisho wetu katika Kijito cha ibada ya kristo na uanafunzi uliobadilisha ulimwengu. Katika uamuzi wangu, hili linaweza kufanyika kwa umuhimu wa kiinjili kuhodhi yale ya mapokeo makuu, kile kiini cha imani na desturi ambayo ni chanzo cha mapokeo yetu yote, kama ni katoliki, Orthodox,

Made with FlippingBook Digital Publishing Software