Theolojia Katika Picha

/ 3 1

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)

7. Tafuta kuelezea: • Vifungu ambavyo havieleweki kwa kauli zinazoleta maana zaidi • Sehemu za ishara kwa mafundisho ya Maandikoyaliyoainishwa • Agano la Kale kwa kutumia Agano Jipya

8. Z ingatia muktadha wote wa kitabu na vifungu vya Maandiko ambamo andiko lolote husika linapatikana.

9. M tambue mwandishi wa kibinadamu na hadhira iliyokusudiwa. Anza kwa kujaribu kugundua nini mwandishi alikuwa anajaribu kusema kwa hadhira yake ya mwanzo. “kifungu cha Maandiko hakiwezi kumaanisha kile ambacho hakijawahi kumaanisha”

Kuelewa Hali ya Mazingira ya Asili

10. T umia taarifa kuhusu maandishi ya kale, lugha, sarufi, muundo wa fasihi, na utamaduni ili kugundua maana iliyokusudiwa ya mwandishi.

11. Z ingatia sana tanzu na vyanzo vya lugha zilizotumiwa na mwandishi, kisha tafsiri Maandiko kwa usahihi, hili linamaanisha tunachukua maana ya wazi ya lugha kama ambavyo huwa inatumika katika tanzu hiyo

12. T afuta mawazo, maadili na kweli ambazo hadithi inaamuru, au unabii unajaribu kuwasilisha. Tafuta kueleza kanuni hizo katika njia ambayo ni kweli na ina manufaa kwa watu wote, kwa wakati wote na hali zote.

Kutafuta Kanuni za Jumla

13. T umia andiko kutafsiri andiko. Ili kuelewa kila sehemu binafsi ya andiko, linganisha sehemu hiyo ya Maandiko na ujumbe wa Biblia nzima. Baada ya kuwa uelewa huu umefikiwa, mtu inabidi atafsiri upya uelewa wake wa andiko zima (theolojia na fundisho) kulingana na ufahamu wa taarifa mpya uliyopatikana kutoka kwenye kifungu hicho cha Maandiko(duara la kihamenetiki)

Made with FlippingBook Digital Publishing Software